Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akipata maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa RAHCO na TRL, Masanja Kadogosa kuhusu mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa ya standard gauge kutoka jijini Dar es alaam hadi mkoani Morogoro alipokuwa anaanza ziara yake ya kutembelea mradi huo. Picha na Geofrey Adroph
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akifafanuliwa jambo na mtaalamu wa mradi kutoka nchini Uturuki wakati wa ziara yake ya kukagua awamu ya kwanza ya ujenzi wa reli ya kisasa ya standard gauge itakayojengwa kutoka jijini Dar es alaam hadi mkoani Morogoro katika eneo la Soga wilayani Kibaha mkoani Pwani.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akioneshwa jinsi mradi utakavyokuwa katika eneo la Soga alipotembelea na kuangalia awamu ya kwanza ya ujenzi wa reli ya kisasa ya standard gauge itakayojengwa kutoka jijini Dar es alaam hadi mkoani Morogoro.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akizungumza na waandishi kuhusu serikali inavyosimamia hatua zote za ujenzi wa wa reli ya kisasa ya standard gauge itakayokuwa chachu ya ukuaji wa viwanda mbalimbali hapa nchini mara baada ya kukamilika wakati wa ziara aliyoifanya eneo la Soga wilayani Kibaha mkoani Pwani.
Mtendaji Mkuu wa Kampuni hodhi ya rasilimali za reli Tanzania (RAHCO) na TRL, Masanja Kadogosa akizungumzia na waandishi wa kuhusu kampuni hiyo inavyosimamia mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa ya standard gauge itakayojengwa kutoka jijini Dar es alaam hadi mkoani Morogoro wakati wa ziara ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa.
Ujenzi wa awali wa ujenzi wa reli ya kisasa ya standard gauge ukiendelea eneo la Soga wilayani Kibaha mkoani Pwani.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akimsikiliza mmoja wa wananchi waliosimamisha msafara wake na kueleza kero wanazokumbana nazo hasa upatikanaji wa kazi ndani ya mradi huo wakati wa ziara ya ukaguzi wa awamu ya kwanza ya ujenzi wa reli ya kisasa ya standard gauge katika eneo la Soga.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akizungumza na wananchi wa eneo la Soga mara baada ya kusikiliza kero zao waliposimamisha msafara wake uliokuwa unakagua mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa ya standard gauge itakayojengwa kutoka jijini Dar es alaam.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Soga wilayani Kibaha wakiwa wameshika bango wakati wa ziara ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa alipokuwa anakagua mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa ya standard gauge.
Msafara wa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, wafanyakazi wa Kampuni hodhi ya rasilimali za reli Tanzania (RAHCO) pamoja na waandishi habari wakielekea kwenye mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa ya standard gauge itakayojengwa kutoka jijini Dar es alaam hadi mkoani Morogoro ambayo ni awamu ya kwanza.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemtaka Mkandarasi Yapi Merkezi na Motaengil Africa anayejenga Reli ya kati ya kisasa (Standard Gauge) sehemu ya Dar es Salaam hadi Morogoro kilomita 205 kuhakikisha ujenzi huo unakamilika ndani ya miezi thelathini iliyopangwa.

Akizungumza mara baada ya kukagua tuta litakapojengwa reli hiyo kutoka pugu, soga hadi ngerengere profesa mbarawa amepongeza kazi inayoendelea na kumtaka mkandarasi kuongeza kasi ili kazi ya kutandika reli ianze katika muda mfupi ujao.
“Hakikisheni kazi ya ujenzi wa tuta na kiwanda cha kutengeneza mataruma ya zege vinakamilika katika muda wa miezi mitatu kutoka sasa ili kwenda na ratiba ya ujenzi huo,” amesema Profesa Mbarawa.

Profesa Mbarawa amekagua kiwanda cha kutengeneza mataruma ya zege yatakayotumika katika ujenzi wa reli hiyo na kusisitiza umuhimu wa mkandarasi kutoa fursa za ajira kwa wananchi wanaozunguka reli hiyo.

“Wale mtakaopata ajira katika reli hii hakikisheni mnafanyakazi kwa bidii na uaminifu ili kuwezesha ukenzi kuwa katika ubora unaotakiwa na kukamilika kwa wakati”, amesisitiza profesa Mbarawa.

Profesa Mbarawa amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli (TRL) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli RAHCO) Bwana Masanja Kadogosa kuanza mchakato wa kuagiza vichwa vipya vya treni vinavyowiana na Reli hiyo ili reli itakapokamilika kusiwe na hoja ya kusubiri vichwa hivyo.

Aidha amesisitiza umuhimu wa TRL na RAHCO kuandaa wataalam watakaotumika kuendesha Reli hiyo ya kisasa kwa kuwapatia mafunzo ya kiufundi na kibiashara ili kuhakikisha utendaji wa Reli hiyo unakuwa wenye tija.
Ujenzi wa Reli ya kisasa ya kati (Standard Gauge) awamu ya kwanza inayoanzia Dar es Salaam hadi Morogoro yenye urefu wa Kilomita 205 unatarajiwa kukamilika 2019 na Serikali inaendelea na juhudi za kuhakikisha inapata fedha ya Ujenzi wa sehemu ya Morogoro-Dodoma.

Zaidi ya Kilomita 2600 za Reli ya Kisasa (Standard Gauge) ZINATARAJIWA kujengwa kutoka Dar es Salaam –Morogoro-Dodoma –Tabora-Isaka-Mwanza na Tabora –Kaliua-Kigoma ili kuiunganisha Tanzania nan chi jirani na hivyo kuboresha huduma za uchukuzi na biashara.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: