Thursday, September 28, 2017

ASILIMIA 75 YA NCHI WANACHAMA WA INTERPOL, YAKUBALI KUJIUNGA PALESTINA KATIKA TAASISI HIYO

Mkutano Mkuu wa Taasisi ya Polisi wa kimataifa wa kuzuia uhalifu wa kijinai “Interpol”, umekubali kujiunga kwa Palestina katika taasisi hiyo,baada ya nchi wanachama 75 kulipigia kura ya ndio azimio hilo. Interpol imethibitisha kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa, Palestina na visiwa vya Solomon kuanzi sasa ni miongoni mwa wanachama wake.

Interpol ni taasisi kubwa zaidi ya kipolisi wa kimataifa iliyoasisiwa mwaka 1923, inajumuisha masuala ya nchi wanachama 190, huku makao makuu yake yakiwa mjini Lyon nchini Ufaransa.Aidha Interpol imekubali uanachama wa Palestina mnamo siku ya jumatatu iliyopita jioni kufuatia ombi la nchi hiyo, kabla ya kulijumuisha katika ajenda zake zitakazopigiwa kura katika Mkutano wake Mkuu,ambao uliketi nchini China Jumatano iliyopita na kuikubalia Palestina ombi lake hilo.

Kwa upande mwingine, Israeli na Marekani zilijaribu kukwamisha hatua hiyo ya kukubaliwa uanachama wa Palestina katika Interpol, kwa kutumia mashinikizo kadhaa juu ya taasisi hiyo ili isikubali ombi la Palestina kuwa mwanachama.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu