Balozi wa China aliyemaliza Muda wake nchi, Dk.Lu Youqing akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarsit Ndikilo wakati wa Mkuu wa Mkoa huyo na Viongozi wa Mkoa huo walivyokwenda kumuaga Balozi wa China aliyemaliza muda wake.

 Balozi wa China aliyemaliza Muda wake nchi, Dk.Lu Youqing akipokea zawadi ya Cheti cha kutambua mchango wa serikali ya China kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo leo jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa China aliyemaliza Muda wake nchi, Dk.Lu Youqing akipokea zawadi ya kinyago cha Twiga kutoka kwa Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega ikiwa ni kutambua mchango wa balozi huyo kwa wananchi wa Mkuranga kwa misaada mbalimbali.
Balozi wa China aliyemaliza Muda wake nchi, Dk.Lu Youqing akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa wa Pwani pamoja na watendaji wa Ubalozi huo leo jijini Dar es Salaam.(picha na Emmanel Massaka , Globu ya Jamii).

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Balozi wa China, Dk. Lu Youqing ametoa msaada wa mashine ya X-Ray katika Hospitali ya Wilaya Mkuranga iliyotokana na ombi la Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega.

Akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo , wakati walikwenda kumuaga Balozi wa China nchini Dk. Lu Youqing ambaye amemliza muda wake nchini.

Katika mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Ndikilo Balozi huyo amemshukuru Rais Dk. John Pombe Magufuli katika ajenda ya Tanzania ya viwanda na maendeleo ya wananchi.

Amesema kuwa maendeleo ya viwanda yataboresha hali ya uchumi wa nchi pamoja na wananchi kutokana na viwanda vitavyojengwa.

Balozi huyo amewahakikishia viongozi wa Mkoa wa Pwani ataendelea kuwa ushirikiano na kuwaomba waendelee kuwasaidia wawekezaji mbalimbali wanaokwenda kuwekeza mkoa huo wasipate usumbufu na hivyo kuharakisha maendeleo ya wananchi.

Aidha Dk. Lu ametoa shukurani katika ushirikiano wa miradi maendeleo ya Viwanda,afya,maji na Elimu.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo na Mbunge wa Mkuranga na Abdallah Ulega leo kwa niaba ya wananchi wa Mkoa wamemshukuru kwa ushirikiano mzuri Balozi wa China wa China aliyemaliza muda wake..

Mkuu wa Mkoa wa Pwani na mbunge wa Mkuranga walimtakia Balozi wa China safari njema ya kurejea nyumbani na kumuomba akawe Balozi wa kuendelea kuitangaza Tanzania na Mkoa wa Pwani akiwa nchini mwao.

Abdallah Ulega amesema katika maombi kwa Balozi huyo ni pamoja na kuwasaidia kufanya ukarabati hospitali ya wilaya Mkuranga.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: