Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Mussa Iyombe akitoa hotuba wakati akifunga kikao cha pamoja kati ya Wadau wa Elimu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais TAMISEMI katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma leo.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Sylvia Temu akitoa maelezo ya awali kuhusu kikao cha Wadau kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi ambaye ni Katibu Mkuu OR TAMISEMI wakati wa kufunga kikao cha Wadau wa Elimu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais TAMISEMI katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma leo.
Mwakilishi wa Wadau wote wa Maendeleo nchini Tanzania (toka Uingereza - DfID) Bi.Janeth Tanya akitoa maelezo mafupi kwa niaba ya Wadau kabla ya ufungaji wa kikao kati ya Wadau wa Elimu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais TAMISEMI katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma leo
Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Elimu Bw. Tixion Nzunda akitoa maelezo ya awali kabla ya hotuba ya Mgeni Rasmi Katibu Mkuu OR TAMISEMI wakati wa kufunga kikao cha Wadau wa Elimu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais TAMISEMI katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma leo.
Mwakilishi wa Wanafunzi, Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Uhuru Dodoma Manispaa darasa la sita Sylvester Allen akipeana mikono na Mgeni Rasmi wakati wa ufunguji wa kikao kati ya Wadau wa Elimu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais TAMISEMI katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma leo
Baadhi ya Washiriki walioshiriki kikao cha kikao cha Wadau wa Elimu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais TAMISEMI katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma leo.

Na. Nteghejwa Hosseah- TAMISEMI

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandishi, Musa Iyombe amesema Serikali itahakikisha inatekeleza maazimio yote yaliyopitishwa kwenye Mkutano wa pamoja wa mwaka wa wadau wa Elimu uliofanyika kwa siku nne Mjini Dodoma.

Eng. Iyombe ameyasema hayo wakati wa kufunga Mkutano wa mwaka wa wadau wa Elimu wenye lengo la kujadili changamoto, mafanikio ya Elimu na kuona namna gani kama wadau wanaweza kutafuta njia ya pamoja ya kuboresha Mfumo wa utoaji wa Elimu Tanzania.

“Nimepokea maazimio yote ya Mkutano huu na nitayawasilisha panopo husika kwa ajili ya Utekelezaji lakini pia niwapongeze kwa kazi kubwa mliofanya, kuanzia wataalamu kutoka Serikalini, sekta binafsi, Mashirika yasiyo ya kiserikali na wadau wa Elimu, hakika mmefanya kazi kubwa na kupitia Mkutano huu tutaona mabadiliko makubwa katika Sekta hii muhimu” alisema Iyombe.

Akitoa salamu za Wizara Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Sylivia Temu amesema Kikao kimekuwa na tija kwa kuwa pamoja na mambo mengine kimejadili masuala yanayotokana na utafiti wa elimu na kwamba matokeo ya tafiti yaliyo onesha changamoto yatafanyiwa kazi kwa pamoja kati ya serikali, wadau wa maendeleo wakiwepo mashirika yasiyo ya serikali.

Wadau wa Elimu nchini wamekutana mkoani Dodoma katika ukumbi wa Hazina kwa muda wa siku tano ikiwa ni juma la elimu Tanzania na kuajadili kwa pamoja chanagamoto na mikakati yakuboresha elimu ili kumtoa mtoto wa kitanzania katika elimu duni.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: