Na Mwandishi Wetu

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imeagiza kuwa mali zote zilizokamatwa katika tukio la wizi wa mafuta katika jahazi MV JITAZAME lililokutwa katika eneo la Bahari Kuu, Kigamboni zitaifishwe. 

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, G.A. Mwambapa ameagiza kwamba mali hizo ambazo ni pamoja na mafuta ya dizeli lita 15,570 iliyokutwa kwenye mapipa 50 na madumu 107 ndani ya jahazi hilo, boti, injini na pampu mbili za maji zitaifishwe kwa manufaa ya Serikali.

Awali akisomewa mashitaka, Kassim Ally Mfaume (49), Mkazi wa Unguja, Zanzibar, ambaye alikuwa Nahodha wa Jahazi hilo, aliieleza Mahakama kuwa mafuta hayo yanayokadiriwa kuwa na thamani ya shilingi milioni thelathini, aliyanunua pamoja na wenzake katika meli moja eneo la Bahari Kuu na kuyaleta Kigamboni ili kutafuta wanunuzi.

Mahakama ilimtia hatiani mshtakiwa kwa kosa la kukutwa na shehena hiyo ya mafuta isivyo halali kosa ambalo mshatakiwa alikiri na kuadhibiwa kifungo cha miezi 18 au kulipa fani ya Tsh 1,000,000/=. Mshatakiwa alilipa faini na kuachiwa huru. 

Mbali na mafuta hayo, Jahazi hilo pia lilikutwa na pump mbili za maji aina ya ‘Hitachi’ na injini moja aina ya ‘Yamaha’ (HP 60). 

Uchunguzi wa awali wa polisi ulibaini kwamba Jahazi hilo MV Jitazame lenye usajili wa Zanzibar (Z – 1006) linamilikiwa na Bw. Ujude Abasi ambaye ni mkazi wa Unguja, Zanzibar.

Tukio la kukamatwa kwa shehena hiyo lilitokea mapema mwezi Agosti, mwaka huu majira ya saa 12.00 asubuhi ambapo askari wa TPA baada ya kupokea taarifa za kuwepo kwa jahazi lenye shehena kubwa ya mafuta likitokea Bahari Kuu kwenda eneo la Ferry-Kigamboni, walilifuatilia na kulikamata likiwa na shehena hiyo. 

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania, inatoa tahadhari kwa watu wote ambao wana tabia ya kuingia maeneo ya bandari kwa lengo la kuiba mali za wateja, kuacha mara moja kwani vifaa vya ulinzi na usalama vilivyopo bandarini hivi sasa ni vya kisasa ambavyo vina uwezo wa kubaini wezi katika maeneo yote ya bandari. Tunawasihi kuithamini na kuilinda rasilimali hii muhimu kwa nchi yetu ambayo inatumika si kwa nchi yet utu bali na majirani zetu wanaotegemea kupitisha mizigo yao katika bandari yetu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: