MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, leo amekiongoza kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar.

Kikao hicho cha kawaida kimefanyika kwa mafanikio makubwa katika ukumbi wa ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi Zanzibar Ndg Waride Bakari Jabu, pamoja na mambo mengine kilipokea na kujadili majina ya wagombea 50 waliojitokeza kuomba nafasi za Uenyeviti CCM Wilaya 12 za Unguja na Pemba na kutoa mapendekezo yake ili kuyapeleka katika vikao husika.

Aidha kikao hicho kilimpongeza Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kufanya ziara ya Chama na Serikali kwa wakati mmoja kufuatilia Utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015-2020 Unguja na Pemba kwa mafanikio makubwa .

Kwa upande wake Rais za Zanzibar aliwashukuru viongozi, watendaji na wananchi mbalimbali walioshiriki katika ziara yake na kusisitiza juu ya umuhimu wa viongozi wa Chama na Serikali kuteremka chini kwa wananchi na kushirikiana nao katika harakati za maendeleo kubaini changamoto zilizopo na kazipatia ufumbuzi .

Dk Sheni alimalizia kwa kusema viongozi wa Chama na Serikali wana wajibu mkubwa wa kutimiza wajibu wao kikamilifu katika kukiwezesha Chama na Serikali kuendelea kukubalika zaidi kwa wananchi na kushinda kwa kiwango cha juu zaidi katika uchaguzi mkuu ujao.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: