Monday, September 25, 2017

MARUFUKU KUTOA MUHIMBILI KUTOA RUFAA KWA MGONJWA ANAYEWEZA KUPATIWA MATIBABU TANZANIA- UMMY MWALIMU

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (katikati) akizindua vyumba viwili vya upasuaji wa watoto wadogo leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Wood na Archie, Sir. Ian Wood na maofisa wengine wakiwa kwenye uzinduzi huo leo.
---
Katika uzinduzi huo Waziri Mwalimu ameitaka Muhimbili kutokutoa rufaa kwa mgonjwa yoyote ambaye anaweza kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo.

“Narudia tena, hata kama ni mimi au kiongozi yoyote asipewe rufaa kama ugonjwa wake unaweza kutibiwa hapa, mimi naweza kuja hapa nikawashinikiza mnipeleke nje, msikubali, simamieni taaluma yenu. Kama madaktari wamezibitisha mgonjwa anaweza kutibiwa hapa, hakuna haja ya kupelekwa nje,” Mhe. Ummy.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu