Washiriki wa mafunzo kutoka Asasi za Kiraia za Visiwani Zanzibar, wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kutawanyika kila kundi kuelekea katika vijiji viwili tofauti vya Msowelo na Matombo kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo. 
Kundi lililokuwa likielekea Msowelo likipiga picha ya pamoja mbele ya gari lao
Kundi lililokuwa likielekea Msowelo likipiga picha ya pamoja mbele ya gari lao
Kundi lililokuwa likielekea Matombo likipiga picha ya pamoja mbele ya gari lao.
Asasi za Kiraia kutoka Zanzibar zimeendelea na mafunzo ya siku mbili kuhusu Utetezi na Ushawishi wa Sera mkoani Morogoro. Asasi mbalimbali kutoka Zanzibar na Pemba ziko katika ziara ya Mafunzo iliyoratibiwa na Foundation for Civil Society (FCS) chini ya mwamvuli wa Association of Non Governmental Organizations of Zanzibar (ANGOZA) inakutanisha wawakilishi Zaidi ya 40 kutoka Zanzibar ambao wamekuja kujifunza namna mashirika ya MVIWATA (Muungano wa Vikundi vya Wakulima Wadogo Tanzania) na MPLC (Morogoro Para-Legal Center). 

Katika siku ya pili washiriki hawa wamepata fursa ya kwenda uwandani ili kukutana na wanufaika wa kazi mbalimbali zinazofanywa na MVIWATA na MPLC. MVIWATA imewapeleka washiriki wilayani Kilosa katika kijiji cha Msowelo ambapo kijijini hapa kumekuwa na migogoro ya Wkulima na Wfugaji ambapo kijijini hapa MVIWATA imefanikiwa kutumia mtandao wake wa msingi kupaza sauti kwa serikali ili kutenga maeneo ya wakulima. Tayari wilayani hapa kuna mashamba 9, ambayo yamefutwa na yamekabidhiwa katika mamlaka ya wilaya ili yagawiwe kwa wananchi.

Kwa upande wa MPLC yenyewe inawaonesha washiriki hawa kazi zao katika eneo la Matombo ambako huko pia MPLC inafanya kazi za utetezi wa haki za umiliki wa ardhi kwa makundi mbalimbali yanayokabiliwa na changamoto hiyo. Shirika hilo limejizolea sifa kwa kazi zake mkoani Morogoro na pia ni shirika kongwe ambalo linafanya kazi za utetezi na ushawishi mkoani Morogoro.

Washiriki kutoka Zanzibar wanatumia nafasi hii kubaini changamoto mbalimbali zinazoyakumba makundi mbalimbali katika jamii ilhali kukiwa na mapungufu katika sera na maamuzi hali inahyowahitaji wananchi kufanya ushawishi na utetezi wa haki za kila kundi ili kuchochea jamii kubaki ikiishi kwa mani na ikiendesha maisha kwa mafanikio.Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Msingi Msowelo, Zainab Kisegele, akizungumza na wanaasasi za Kiraia kutoka Visiwa vya Zanzibar,wakati walipofika kijijini hapo Msowelo kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo kujifunza namna ya kupambana na changamoto za migogolo ya Ardhi na njia wanazoweza kutumia kutatua migogolo katika Kata za Vijiji.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Msingi Msowelo, Ally Omary, akizungumza na wanaasasi za Kiraia kutoka Visiwa vya Zanzibar,wakati walipofika kijijini hapo Msowelo kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo kujifunza namna ya kupambana na changamoto za migogolo ya Ardhi na njia wanazoweza kutumia kutatua migogolo katika Kata za Vijiji.Washiri wakisikiliza kwa umakini
Picha ya pamoja baada ya mafunzo kwa walioelekea Kijiji cha Msowelo


Washiriki waliokuwa wakielekea Matombo wakiwa katika gari kuelekea katika mafunzo kwa vitendo.
Wakiwa katika mafunzo
Wakiuliza maswali kwa wenyeji wao ili kujifunza zaidiMafunzo yakiendelea Matombo.....Mafunzo yakiendelea Matombo.....


Ushuhuda .......

Picha ya pamoja baada ya mafunzo kwa walioelekea Kijiji cha Matombo.Baada ya mafunzo kwa pande zote mbili Msowelo na Matombo, washiriki walikutana tena na kuungana kwa majadiliano baada ya mafunzo kwa vitendo


Washiriki wakijielezea jinsi walivyoweza kujifunza kutoka kwa wenzao walokokwenda.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: