Tuesday, September 5, 2017

MWILI WA MWANDISHI WA HABARI, MUHINGO RWEYEMAMU WAAGWA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA, MAZIKO YAFANYIKA MAKABURI YA KINONDONI.

Mwili wa marehemu mwandishi wa habari mkongwe nchini, Muhingo Rweyemamu ukiwa uwanja wa mnazi mmoja kwa ajili ya kuagwa.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe akiongoza waombolezaji katika kuaga mwili wa marehemu mwandishi wa habari mkongwe nchini, Muhingo Rweyemamu yaliyofanyika leo Uwanja wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Marehemu Muhingo Rweyemamu amezikwa leo kwenye makaburi ya Kinondoni.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akitoa neno wakati wa  kumuaga Mwandishi wa habari mkongwe nchini, Muhingo Rweyemamu yaliyofanyika leo Uwanja wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Mtoto wa marehemu akisoma risala.
Mwili wa marehemu mwandishi wa habari mkongwe nchini, Muhingo Rweyemamu ukiingizwa uwanja wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Waombolezaji wakiwa katika uwanja wa mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Tanga Godwin Gondwe akitoa machache.

Familia na viongozi waliowahi kufanyakazi na marehemu mwandishi wa habari mkongwe nchini, Muhingo Rweyemamu.
Mhariri Mtendaji wa kampuni ya New Habari, Absalom Kibanda akitoa neno la shukrani kwa wanaombolezaji.
Viongozi na waombezaji wakioaga mwili wa marehemu.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe akiongea na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda mara baada ya kuaga mwili wa marehemu.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe akisalimiana na mwandishi mkongwe Hamis.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu