Marehemu Mohamedi Idi Mturuma (Muddy)

Umoja wa Tanzania Ujerumani(UTU) ukishirikiana na watanzania wanaoishi Ujerumani na Spain ,unawajulisha ndugu,jamaa,marafiki ,wapenzi na watanzania wote kuwa mwili wa msanii marehemu Muhamedi Iddi Mturuma aka MUDDY utasafirishwa siku ya ijumaa 29-09-2017 na utafika siku ya jumamosi 30-09-2017 saa 8.30(saa nane na nusu) Usiku wa kuamkia Jumapili katika uwanja wa ndege wa JKN Dar-es-salaam,mazishi yatafanyika nyumbani kwa marehemu huko Mbezi ya Kimara,na taratibu za maziko mnaweza kupiga simu namba 0653319069 au 0656210725 ili kujua lini mazishi yatafanyika,mwili a marehemu utafuatana na rafiki yake kipenzi msanii Mussa Selemani aka MOSES FAB anayeishi Uingereza .Marehemu Mohamedi Iddi Mturuma "MUDDY" alikuwa anaishi nchini ujerumani na umauti ulimfika siku ya 18.09.2017 nchini Spain ambako alikwenda kufanya shughuli zake za usanii wa sarakasi.
Allah amlaze mahala pema peponi- AMIIN
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: