Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,William Lukuvi akizungumza na watendaji wa wilaya ya Kigamboni kuhu kuvunja rasmi Wakala wa Uendelezaji Mji wa Kigamboni (KDA) leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa wilaya ya Kigamboni,Hashim Mgandirwa akizugumza machachena katika mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya viongozi mbalimbali wakimsikiliza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,William Lukuvi. (Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya jamii.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi ametangaza rasmi kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa John Pombe Magufuli ameivunja rasmi Wakala wa Uendelezaji Mji wa Kigamboni (KDA) kuanzia leo.

Aidha Mheshimiwa Rais ameelekeza kwamba shughuli zote zilizokuwa zinafanywa na KDA sasa zifanywe na manispaa ya kigamboni kwa mujibu wa sheria.

Na kuanzia sasa manispaa ya Kigamboni itahusika kupanga na kusimamia ardhi yake kama manispaa nyingine zinavyofanya, na Wizara ya Ardhi itaendelea kusimamia masuala yote yahusuyo ardhi kwa ujumla wake kama inavyofanya katika manispaa zote nchini.

Waziri wa Ardhi pia akatangaza kwamba kuanzia sasa wakazi wa mji wa Kigamboni wasizuiliwe kupewa hati zao za umiliki wa ardhi na wasizuiliwe kupewa vibali vya ujenzi.

Mheshimiwa Lukuvi pia amefuta mashamba mawili yalioko wilayani kigamboni jijini Dar es salaam na kurudisha mashamba hayo kwa serikali ya wilaya ya kigamboni.

Ufutaji hu ni baada ya wamiliki hao kushindwa kuyaendeleza na kuwanyima fulsa wananchi kufanya shughili zingine na kuinyima wilaya kufanya shuguli za viwanda na uwekezaji mwingine kutokana na kuhodhi kwa maeneo hayo.

Nae mbuge wa wa Kigamboni Dr. Faustine Ndugulile ametoa shukrani zake kwa Rais kwani Muingiliano wa majukumu wa mamlaka hizo ulikuwa ukiwabana wananchi hivyo kuwasababishia kushindwa kufanya shuguli za maendeleo.

Nao baadhi ya wananchi wa Kigamboni wamefurahishwa sana na maamuzi ya Rais kuhusu kuvunjwa kwa Wakala wa Uendelezaji wa Mji wa Kigamboni (KDA) kwani ulikuwa unawapa wakati mgumu katika kuendeleza maeneo yao na kuleta urasimu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: