Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda leo amepokea Magodoro 1,000 yenye thamani ya Shillingi Million 100 kutoka Kiwanda cha utengenezaji wa Magodoro ya Dodoma Asili kwa kushirikiana na Wadau wanaopendezwa na kazi kubwa anayoifanya katika kutatua kero Wananchi.

Makonda amekabidhiwa Magodoro hayo Mjini Dodoma na Kiwanda hicho mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Jordan Rugimbana.

Akizungumza baada ya Makabidhiano hayo Makonda amepiga Marufuku kitendo cha Wagonjwa kulazwa Chini Hospitalini kwakuwa Magodoro hayo yanaenda kutatua kero hiyo.

Amesema kuwa Magodoro aliyopatiwa atayakabidhi kwenye Hospital zote za Mkoa wa Dar es Salaam kwakuwa baadhi zimekuwa na upungufu wa Magodoro hali inayofanya Wagonjwa kulala juu ya Vyuma vya kitanda na wengine kutandika Kanga na Nguo kwenye Sakafu.
Amesema idadi kubwa ya Wananchi wamekuwa wakitoka Mikoani kufuata huduma za Afya Dar es Salaam kuokana na Wingi wa Hospital za Kisasa za Umma na Binafsi hivyo kusababisha Hospital kuwa na Wagonjwa wengi.

Licha ya Changamoto hiyo Makonda amesema Sekta ya Afya jijini Dar es Salaam imeimarika kwa kiasi kikubwa ambapo lengo lake ni kuona Mkoa huo unakuwa kinara kwenye utoaji wa huduma Bora za Afya.

Ameshukuru Kiwanda hicho na Wadau waliomuunga Mkono na kuwasihi Wananchi kununua Magodoro ya Dodoma Asili yanayotengenezwa na Kiwanda cha Wazawa ili kukuza Uchumi wa Taifa.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Jordan Rugimbana amempongeza RC Makonda kwa kazi kubwa anayoifanya katika Sekta mbalimbali ikiwemo Maboresho ya Jeshi la Polis na kusema ataenda Dar es salaam kujifunza namna walivyofanikiwa kwenye Ulinzi na Usalama.

Nae Mkurugenzi wa Kiwanda cha Magodoro ya Dodoma Asili Bwana Haider Gulamali amesema wataendelea kutoa ushirikiano kwa RC Makonda kwakuwa kazi anayoifanya ni kubwa na inawagusa Wananchi wote hususani wanyonge.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: