Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Renata Mzinga (kushoto), akiwavisha beji miongoni mwa wanafunzi 230 waliojiunga na Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), katika hafla iliyofanyika kwenye Uwanja wa Ilulu, Lindi Mjini.PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG.
Mkufunzi Mkuu kutoka TGGA Makao Makuu Dar es Salaam, Emmiliana Stanslaus akitambulishwa wakati wa hafla hiyo.
Young Leader wa Dar es Salaam, Valentina Gonza akitambulishwa wakati wa hafla hiyo
Makamu Mwenyekiti wa TGGA Mkoa wa Lindi, Sharifa Mkwango akijitambulisha.
Mwenyekiti wa Vijana Mkoa wa Dar es Salaam, Ruth Namatanga akimvisha beji mwanachama mpya.
Girl Guides wakitumbuiza wakati wa hafla hiyo.
Katibu wa TGGA Mkoa wa Lindi akimvisha beji mwanachama mpya.
Girl Guides wapya wakila kiapo.
Girl Guides mpya Elvila Dickson akisoma risala.
RPC Mzinga akihutubia wakati wa hafla hiyo.
RPC Mzinga akiwa na baadhi ya viongozi wa TGGA.
RPC Mzinga akiwa na baadhi ya Girl Guide wapya pamoja na viongozi.

Katibu Mkuu wa TGGA Taifa, Grace Macha akiwavisha beji miongoni mwa wanafunzi 230 waliojiunga na Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), katika hafla iliyofanyika kwenye Uwanja wa Ilulu, Lindi Mjini.

Na Richard Mwaikenda, Lindi.

JESHI la Polisi limeahidi kushirikiana na Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), kuwakamata wanaowanyanyasa na kuwabaka Watoto wa Kike.

Kauli hiyo ilitolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Renata Mzinga katika hafla ya kuwaapisha wanafunzi wa kike 230 waliojiunga na TGGA mkoani Lindi jana.

Hilo siyo ombi bali ni wajibu wa jeshi la Polisi kushirikiana na chama hicho pamoja na jamii kuhakikisha wale wote wanaowatendea vitendo vibaya watoto wa kike wanakamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

"Msiombe msaada kwetu, bali sisi tunahitaji sana msaada mkubwa kutoka kwenu, kwani huku kwetu watoto wa kike wanakuja wakiwa wameharibikiwa, ushauri wenu kwao umesaidia sana," alisema Kamanda Mzinga na kuwataka waendelee kutoa elimu hiyo kwenye Tarafa, Kata, Kijiji na vitongoji ili kumkoboa mtoto wa kike.

Kamanda Mzinga, aliipongeza TGGA kwa kitendo cha kuwapatia mafunzo takribani wasichana 1200 ya jinsi ya kuepukana na vitendo vibaya vya kubakwa na kupewa mimba, magonja kama vile Ukimwi na ndoa za utotoni.

Akielezea walichonufaika katika wakati wa mafunzo yaliyodumu kwa takribani siku nne, Mwenyekiti wa TGGA Mkoa wa Lindi, alisema kuwa waischana walifaidika kwa kupata mafunzo ya ukakamavu, kujiamiini, kuepukana na vikwazo mbalimbali wanavyokumbana navyo wakati wa kwenda shule na kurejea nyumbani ikiwemo kurubuniwa kwa kupewa mimba za utotoni.

Alitaja mambo mengini waliyonufaika nayo ni ujasiriamali, utunzaji wa mwili, utunzaji wa mazingira, uongozi, maadili, kujitolea , kuwa na upendo na uzalendo kwa nchi yao.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: