Shirika la MajiSafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO), linawatangazia wakazi wa jiji la Dar es Salaam pamoja na Miji ya Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani kuwa kutakua na operesheni maalum ya kusitisha mara moja huduma ya MajiSafi kwa wateja wake wote ambao wanamalimbikizo ya madeni kama ifuatavyo;

• Wateja wenye madeni ya bili za Maji kuanzia mwezi mmoja na kuendelea

• Wateja waliofanya malipo NUSU (part payment) katika bili zao Maji za mwezi

• Pamoja na wateja wote wenye madeni ya muda mrefu na sugu

Operesheni hii imeanza rasmi hivyo Dawasco inawataka wateja wake wote kulipia bili zao za huduma ya Majisafi pamoja na madeni ya kipindi nyuma mapema ili kuepuka usumbufu wakusitishiwa huduma ya Majisafi katika makazi yao.

Kwa wateja ambao hawajapata bili zao za Maji za mwezi kupitia ujumbe mfupi wa simu (sms) wanaweza kuwasiliana na Dawasco huduma kwa wateja kwa namba 0800110064 (Bure) au wafike ofisi ya Dawasco karibu nao kwa msaada zaidi.

Kumbuka ukisitishiwa huduma gharama ya kurudisha ni Tsh 30,000/= lipia sasa kuepuka usumbufu huu

IMETOLEWA NA:
OFISI YA UHUSIANO
DAWASCO-MAKAO MAKUU.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: