Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainabu Telack akipokelewa na baadhi ya Watumishi wa Shirika la Ndege la Precision Air na Kampuni ya Acacia , alipowasili katika uwanja wa ndege wa Kahama, mkoani Shinyanga wakati a uzinduzi wa safari za Precision mkoani humo. Nyuma yake ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Fadhili Nkulru.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack akikata uteope kuashiria uzinduzi rasmi wa safri za ndege za Shirika la Precision Air Tanzania Plc kati ya Dar es Salaam na Kahama, Mkoani Shinyanga. Wengine ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Fadhili Nkurlu (mwenye kofia) na Meneja Uratibu na Mahusano wa Precision, Hillary Mremi (kulia).
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainabu Telack akijadiliana na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Fadhili Nkurlu (mwenye kofia) wakati wa uzinduzi wa safari za ndege za shirika la Precision Air kati ya Dar es Salaam na Kahama, mkoani Shinyanga. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Meneja Mratibu na Mahusiano wa Precision Air, Hillary Mremi akiwafafanulia jambo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainabu Telack na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Fadhili Nkurlu (kulia), wakati wa uzinduzi wa safari za ndege za shirika hilo wilayani Kahama.
Marubani wa Precision Air wakiteremka kutoka kwenye ndege hiyo mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kahama, mkoani Shinyanga, ambapo ulifanyika uzinduzi rasmi wa safari za shirika hilo wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Fadhili Nkurlu (mwenye kofia) akisalimiana na marubani wa ndege ya Precision wakati ilipotua katika uwanja wa Kahama, ambako ulifanyika uzinduzi rasmi za safari za kati ya Dar es Salaam na Kahama, mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainabu Telack (mwenye ushingi) na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Fadhili Nkurlu (mwenye kofia) wakiwa katika picha ya pamoja wafanyakazi wa shirika la ndege la Precision Air Tanzania na kampuni ya Acacia.

Shirika la Ndege la Kitanzania Precision Air Services Plc, leo limeanza rasmi safari kati ya Dar es Salaam na Kahama, Mkoani Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinynga amepongeza shirika hilo kw kunzisha  safari za mkoni humo kwa kuwa ni fursa nzuri kwa wakzi wa mkoa huo pmoja na wawekezaji wanotaka kuwekeza katika mkoa huo.

Akizungumza baada ya ndege hiyo kutua katika uwanja wa ndege wa Kahama uliokuwa ukimilikiwa na kampuni ya uchimbaji dhahabu ya Acacia, Telack amesema, shirika hilo limefungua nia kwa wawekezaji wngi hasa kwa kuzingatia wanahitaji usafiri wa uhakika ili wweze kufnya kazi zao vizuri.

“Hii itaondoa usumbufu uliokuwepo zmani wa mtu akitaka kwenda Dar es Salaam lzima aende Mwanza, sasa hivi hata wawekezaji na wafanyabiahara wanaweza kuja moja kwa moja, ni fursa nzuri kwetu,” amesema Telack.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: