Mshindi wa kwanza katika mashindano ya uandishi bora wa habari za sayansi na kilimo (Biotchnolojia) katika kuendeleza Kilimo, Gerald Kitabu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako mara baada ya kumkabidhi cheki ya Dola 1500 kwa kuwa mshindi wa mashindano ya uandishi bora wa habari za Sayansi makabidhiano hayo yamefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Tume ya Sayansi (Costech) jijini Dar es Salaam leo.
---
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako leo amekabidhi vyeti na Zawadi mbalimbali kwa waandishi wa habari waliofanya vizuri katika kuandika habari za Sayansi kwa mwaka 2017.

Akizugumza mara baada ya kutoa tuzo hizo jijini Dar es Salaam, Waziri Ndalichako pamoja na kuwapongeza wanahabari pia ameitaka Tume ya Taifa ya Sayansi (COSTECH) kuendelea kutoa ushirikiano kwa wanahabari ili habari zinazoandikwa ziwe sahihi, zenye lugha nyepesi ili ujumbe uweze kufika kwa jamii kwa ufasaha.


Katika tuzo hizo Mshindi wa Kwanza amezawadiwa cheki ya Dola 1500, wapili dola 1200 na watatu Dola 1000 na wengine Dola 750, 375 na 250 pia baadhi ya Vyombo vya habari wamezawadiwa cheti cha Shukrani kwa kuchapisha kazi za Sayansi na Kilimo.

Ukiacha Gerald Kitabu wengine ni Kelvin Gwabara, Innocent Mugune, Coletha Makurwa, Shadrack Sagati, Elias Msuya, Fatma Abdul, Lucy Ngowi, Restuta Damian, Heren Kwavava, Daniel Sembelya na Zakaria Gabriel.
Baadhi ya washindi wa Tuzo za uandishi mahiri wa habari za Sayansi na Kilimo (Bioteknolojia) wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Elimu ,Sayansi,Teknolojia na Ufundi Prof. Joyce Ndalichako na Mkurugenzi Mkuu wa Costech, Hassan Mshinda katika hafla ya kuwazawadia washindi wa habari waliofanya vizuri zaidi kwenye kuandika na kuelimisha umma kuhusu matumizi ya Sayansi, Teknologia na ubunifu hususani Bioteknologia katika kuendeleza kilimo.
Baadhi ya waandihsi wa habari waliofika katika hafla fupi kuwakabidhi tuzo za uandishi mahiri wa habari za Sayansi (Biotechnology) jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Elimu, Sayansi,Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako akizungumza wakati wa hafla hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako akimkabidhi Hellen Kwavava hundi yake wakati aliposhinda tuzo ya uandishi bora wa habari za Sayansi na kilimo kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Costech, Hassan Mshinda katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Costech jijini Dar es salaam leo.
Waziri wa Elimu , Sayansi,Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako akimkabidhi Kelvin Gwabara tuzo yake wakati aliposhinda tuzo ya uandishi bora wa habari za Sayansi na kilimo kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Costech, Hassan Mshinda katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Costech jijini Dar es salaam leo. Mkurugenzi Mkuu wa Costech, Hassan Mshinda
Waziri wa Elimu , Sayansi,Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako akimkabidhi hundi ya Dola 750 wakati aliposhinda tuzo ya uandishi bora wa habari za Sayansi na kilimo kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Costech, Hassan Mshinda katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Costech jijini Dar es salaam leo.
Waziri wa Elimu , Sayansi,Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa tuzo za uandishi bora wa habari za Bioteknologia baada ya kukabidhiwa tuzo ya uandishi bora wa habari za Sayansi na kilimo kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Costech, Hassan Mshinda katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Costech jijini Dar es salaam leo.
Mkurugenzi wa TBC, Ayoub Rioba akizungumza katika hafla ya utoaji tuzo za uandishi bora wa habari za Sayansi na Kilimo jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Elimu , Sayansi,Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako, Mkuu Mkuu wa Tume ya Sayansi na Technologia, (COSTECH), Hassan Mshinda na Mkurugenzi wa TBC wakiwa katika picha ya pamoja na Washindi wa tuzo za umahili bora wa habari za Sayansi na Kilimo jijini Dar es Salaam leo. Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamaii.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: