Dr.Riyad Al-Maliki, ambae ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Palestina, amepongeza hatua ya kuipigia kura ya ndio nchi yake na hatimae kukubaliwa uanachama wa Interpol,kupitia mkutano wake mkuu uliofanyika mjini Beijing nchini China. Amesisitiza kuwa hatua hiyo inathibitisha kuaminika uwezo wa Palestina katika kutekeleza sheria,dhamira halisi na maadili muhimu ya Interpol.

Waziri pia ameashiria kupatikana kwa ushindi huo,kumetokana na msimamo wa awali wa idadi kubwa ya nchi wanachama wa Interpol, iliyotetea sababu ya kuwepo kwa taasisi hiyo na kanuni zake za msingi,pale zilipokataa waziwazi kuupa nafasi ubabe wa kisiasa utawale. Huku waziri akiongeza kusema:" Leo haki na kanuni zimeshinda mambo mengine yote"."Leo, ukweli na kanuni zimeshinda mambo mengine yote.

Dr.Riyad Al-Maliki kwa niaba ya taifa la Palestina,amezishukuru nchi wanachama zilizoiunga mkono Palestina katika jitihada zake,huku akitilia mkazo kuendelea kwa nchi yake katika jitihada za kujiongezea hadhi na nafasi mbalimbali kimataifa,ikiwa ni pamoja na kutetea haki za Wapalestina,uhuru na amani yao kwa njia ya kidiplomasia na kisheria, ikiwa ni pamoja na kujiunga na taasisi husika za kimataifa.

Kwa mnasaba huu pia, Waziri Al-Maliki amesisitiza ahadi ya nchi yake ya Palestina katika kutimiza majukumu yake ya kuchangia kupambana na uhalifu na kuimarisha utawala wa sheria katika ngazi ya kimataifa. Huku ikishirikiana na nchi wanachama wa Interpol katika kukuza hadhi na nafasi ya taasisi hiyo, ushiriki wa kidhati kabisa wa kimataifa dhidi ya uhalifu unaohatarisha maisha wananchi na mustakabali wao duniani.

Aidha ameongeza kusema: "Nchi ya Palestina inauchukulia uanachama huu na majukumu yake kama ni sehemu ya wajibu wake kwa Wapalestina,pia ni wajibu wa kimaadili kwa walimwengu wote. Palestina ipo tayari na inaweza kubeba majukumu na wajibu huu kama mshirika wa dhati katika jamii ya kimataifa,itachangia hasa kuendeleza maadili yetu ya msingi ya pamoja kama mataifa. "
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: