Msanii wa muziki aliyewahi kufanya vizuri na wimbo Malavidavi, Mpenzi Jini na nyingine nyingi, Z Anto, amefunguka kwa kusema kuwa wiki hii ataachia kazi yake mpya huku akidai haamini kama kazi yake hiyo itashindwa kufanya vizuri kwa kuwa Diamond na Alikiba wameachia kazi zao mpya ambazo zinashindanishwa mitandaoni.

Akiongea na waandishi wa habari Jumamosi hii jijini Dar es salaam, Z Anto amedai yeye atapita katikati ya Diamond na Alikiba kwa kuwa muziki wake unapendwa na watu wa rika zote na pia hauna makundi kama ulivyo wa wawili wao.

"Wote nawaweza sana, muziki wangu ni mtamu na hauna makundi kwahiyo kila mtu anaweza kuusikiliza hata hao bila shaka ni mashabiki wa muziki wangu ndio maana nikasema kuogopa kuachia ngoma sasa hivi kwaajili ya Diamond na Alikiba utakuwa ni ujinga," alisema Z Anto.

Aliongeza "Binafsi najiamini sana kwa sababu muziki wangu ni mzuri na tayari kuna platfom ambayo niliiweka toka kipindi cha nyumba sema tu ukimya wangu ndio umewapa nafasi hawa ndugu zangu lakini sioni kama nitatizo kwasababu bado nafasi yangu naiona,"

Muimbaji huyo amesema anajua muziki umebadilika sana ndio maana na yeye amejipanga kuvingine ili kukabiliana na watu ambao wanashindana kwa sasa kwenye muziki.

"Kila mtu anatakua kuwa juu zaidi ya mwenzake na ukimya wangu umewapa nafasi wasanii wengi sana na lengo langu ni kufanya vizuri zaidi ndio maana nikasema sishindani na Diamond wala Alikiba mimi nitapita katikati yao na mashabiki ndio wenye maamuzi ya mwisho katika hili kwahiyo mimi ningesema tusubiri kazi mpya waisapport halafu ndio tuanze kupima," alisema Z Anto.

"Mimi naamini msanii yoyete anaweza kufanya vizuri zaidi ya hata wakongwe kama akijipanga vizuri muziki una sifa hiyo, kwahiyo mimi naweza kusema lolote linaweza kutokea kwenye muziki lisiwe leo au kesho muda ukifika hauwezi kushindana nao, wakati ni ukuta," alifafanua zaidi.

Katika ujio wake muimbaji huyo amesema tayari ameandaa audio na video ambayo itaanza kutoka na kuleta picha mpya katika muziki wake.

"Kazi zipo tayari kwa sababu ni nyingi na naanza na moja moja, siku yoyote kuanzia leo nitaachia kazi moja na baada ya upepo wa hapo nitaendelea kasi hiyo hiyo kadri mambo yanavyokwenda," alisema Z.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: