Afisa huduma kwa wateja wa Benki ya UBA Tanzania, Bi Stella Matau akifurahia kumuhudumia mmoja wa wateja wao wakubwa aliyefika katika benki hio huku benki hio ikiendelea kung'ara katika kutoa huduma bora kwa wateja kwa wakati wote
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya UBA Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wateja wao waliofika katika benki hio kwaajili ya kupata huduma za kibenki
Meneja Uendeshaji wa Benki ya UBA Tanzania, Bw Chriss Byaruhanga (wa Kwanza kushoto) akikata keko na baadhi ya wateja wao ikiwa ni ishara ya kuendeleza shamrashamra za wiki ya huduma kwa wateja ambapo wateja hao wameisifu benki hio kwa kutoa huduma bora wakati na sio kwa kipindi cha kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja.

Wiki ya huduma kwa wateja inaendelea huku benki ya uba tanzania ikiendelea kutoa huduma bora na zenye kutimiza malengo ya wateja wao huku kituo chao cha huduma kwa wateja kikiendelea kushika hatamu kwa wateja wao kwa kuwapa huduma bora masaa 24. Uba Bank ambao hivi karibuni walijidhatiti tena kwa kuanzisha kituo cha huduma kwa wateja kwa masaa 24 wamezidi kuwapatia huduma bora wateja wao bila kuangalia kuwa ni wiki ya huduma kwa wateja wao Hutoa huduma bora siku zote.

Uba bank wanafurahi kuwahudumia wateja wao siku zote huku wiki ya huduma kwa wateja ikiendelea kuwa sehemu tu ya kuendeleza kutoa huduma bora kwa wateja.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: