Monday, October 2, 2017

BONDIA OMARI KIMWERI WA AUSTRALIA ATOA MSAADA KWA KOCHA KINYOGOLI

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimpatia zawadi ya vifaa vya mchezo wa ndondi kocha mkongwe wa mchezo huo, Habibu Kinyogoli 'Masta' vifaa vilivyotolewa na bondia Omari Kimweri anayefanya shughuli zake nchini Australia. Kimweri amekuwa akisaidia sana mchezo wa masumbwi nchini kadri awezavyo. Picha zote na SUPER D BOXING NEWS.
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimpatia zawadi ya vifaa vya mchezo wa ndondi kocha mkongwe wa mchezo huo, Habibu Kinyogoli 'Masta' vifaa vilivyotolewa na bondia Omari Kimweri anayefanya shughuli zake nchini Australia.

Na Mwandishi Wetu.

KOCHA wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amemkabidhi vifaa vya mchezo wa masumbwi kwa kocha mkongwe wa mchezo huo nchini Habibu Kinyogoli 'Masta' vifaa vilivyotumwa na bondia Mtanzania Omari Kimweri 'Lion Boy 'anayefanya shughuli zake nchini Australia.

Vifaa hivyo vya kufundishia vimeletwa na Kimweri kwa ajili ya kufundishia vijana chipkizi wa mchezo wa masumbwi nchini bondia huyo alimpatia Super D ili amwakilishie kwa Kinyogoli kwa kuwa yeye alkikuwa na majukumu mengine.

Super D aliwasilisha vifaa hivyo wa ndondi kwa kocha huyo akizungumza baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo kocha Kinyogoli amesema anamshukuru sana kimweri kwa msaada wako huo kwa kuwa vijana wengi wakienda nje ya nchi awawakumbuki wenzao lakini yeye mara kwa mara amekuwa akinikumbuka kwa kuniletea vifaa vya mchezo wa masumbwi nchini kwa ajili ya kuwaendeleza wenzake.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu