Idara za Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Same zinaendelea na mapambano dhidi ya Madawa Ya Kulevya ambapo tangu tar. 1/10/2017 watu 3 wameshakamatwa. Kati Yao 1 ni Kwa kosa la kukutwa na mirungi kata ya Mhezi na 2 Kwa kosa la kustawisha mirungi Kata ya Kirangare.

Napongeza juhudi hizi zinazofanywa na Kamati.

Na ninaendelea kutoa wito Kwa wananchi wanaofikiri nguvu hii ni ya soda. Wang'oe mirungi.

Tunajua wengi wametii Agizo hili isipokuwa wachache wanaojiita sugu. Tayari waliong'oa mirungi wamepanda mazao mbadala kama tangawizi, kahawa, viazi na mengine.

Tangu Januari, 2017 watu waliokamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria ni zaidi ya 70.

Nawahakikishia wananchi wa Same. Hatutalala Usingizi mpaka mzizi wa mwisho wa mrungi ung'olewe kwenye ardhi ya Same.

Rosemary Senyamule
DC Same.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: