Kaimu RTO mkoa wa Kilimanjaro, ASP Willy Mwamasika. akiwa kayikabayendi kuu ya amkoani Kilimanjaro alipokuwa akitekeleza moja ya majukumu kabla magari hayajaondoka kulelekea mikoani.
Baadhi ya Mabalosi wa usalama barabarani (RSA) wakiwa katika stendi kuu ya mabasi Mkoani Kilimanjaro wakiwa wanatoa elimu kwa abiria kabla ya mabasi kuondoka kuelekea mikoani.
Wakaguzi wa magari na wasaili wa Madereva wakiendesha ukaguzi wa magari stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani Moshi Kilimanjaro leo.Picha na Vero Ignatus Bog.
Wakwanza kushoto ni Mkurugenzi wa barabara Sumatra SACP Johansen Kahatano ASP Willy Mwamasika. Mkurugenzi wa Habari Elimu na Mawasiliano kutoka Taasisi ya Mabalozi wa Usalama kaimu meneja Salum Pazzy Afisa mawasiliano mwandamizi sumatra.
Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa barabara Sumatra SACP Johansen Kahatano ASP Willy Mwamasika. Mkurugenzi wa Habari Elimu na Mawasiliano kutoka Taasisi ya Mabalozi wa Usalama Barabarani, Augustus Fungo.
Koplo Peter akiwa na mabalozi wa usalama barabarani stendi kuu ya mabasi Moshi mkoani Kilimanjaro.
Mabalozi wa Usalama barabarani (RSA) wakizungumza na Ibrahim Shayo (aliyevaa kofia) ambae ni mmiliki wa nabasi ya Ibra Line.
Mabalozi wa Usalama barabarani, Afisa mfawidhi sumatra mkoa wa kilimanjaro Johns Makwale aliyevaa kizibao cha njano wakiendelea kutoa Elimu katika Stendi kuu ya mabasi mkoani Kilimanjaro.
Mkurugenzi uthibiti usafiri wa barabara sumatra SACP Johansen Kahatano,ASP Willy Mwamasika ,Afisa Pazzy kutoka Sumatra wakiendelea kukagua magari katika Stendi kuu ya Mabasi Moshi Kilimanjaro.
Mmoja wa Abiria akiwa amebanda siti ya mbele akiwa amepakata mzigo mkubwa ambao ni hatari kwake na dereva pia kama alivyokutwa leo na Blog hii.
Mabalozi wa usalama barabarani wakiwa katika stendi kuu ya mabasi Moshi mkoani Kilimanjaro wakiendelea kutoa elimu kwa abiria pamoja na makondakta/abiria kuhusiana na Usalama barabarani.
Balozi Elizabeth Maembe akitoa elimu kwenye moja ya mabasi yaendayo mikoani katika stendi kuu ya mabasi Moshi mkoani Kilimanjaro.Picha na Vero Ignatus Blog.

Na Vero Ignatus Blog.

Jeshi la polisi Kitengo cha Usalama barabarani kwa kusirikiana na wadau wa usalama barabarani wamefanya zoezi la  ukaguzi wa magari stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani na kugundua makosa mbalimbali yanayofanyawa na madereva pamoja na makondakta.

Akizungumzia zoezi hilo Kaimu RTO mkoa wa Kilimanjaro, ASP Willy Mwamasika amesema kuwa zoezi hilo ni endelevu na wameliendesha kwa muda mrefu sasa ambapo amesema magari ambayo yamekutwa na makosa yanatozwa faini na mengine Kupelekwa kituoni au kufunguliwa mashtaka .

Amewataka wamiliki wa mabasi yanayosafirisha abiria wanapobadili ratiba zao wakumbuke na kufuta kwenye magari yao ili wasiwachanganye abiria wanaposafirikauli mbiu ya maadhimisho hayo ni "Zuia Ajali Tii Sheria Okoa Maisha".

Mkurugenzi wa Elimu Habari na Mawasiliano kutoka Taasisi ya Usalama barabarani (RSA)Augustus Fungo amesema kuwa zoezi hilo limekuwa zuri kwani limefanyika sambamba na mihimili  mikuu ya usalama barabarani ikiwemo  Polisi,Sumatra na Jeshi la zima moto pamoja na wadau mbalimbali wa usalama barabarani.

Kwa sasa zoezi hili ni msisitizo katika wiki ya nenda kwa usalama barabarani lengo kupeana elimu ya usalama na usafirishaji, kukumbushana wajibu wetu barabarani kwa abiria na dereva, kuwachukulia hatua wale ambao wanavunja sheria za usalama barabarani.

Huku akisema kauli mbiu yao Mabalozi wa Usalama barabarani ni #Safiri Salama Ajali sasa basi#"
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: