Naibu Waziri wa Ujenzi, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Elias John Kwandikwa (kushoto) akifuatilia kwa makini majadiliano wakati wa kupokea maoni ya wadau mbele ya Kamati ya Bunge ya Miundombinu kuhusu Muswada wa Sheria ya Shirika la Mawasiliano Tanzania kwenye kikao kilichofanyika ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni, Dodoma. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Prof. Norman Sigalla King akifafanua jambo kwa wajumbe (hawapo pichani) wa Kamati hiyo.
Naibu Katibu Mkuu wa Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Angelina Madete (aliyekaa katikati) akifuatilia majadiliano ya wadau kuhusu Muswada wa Sheria ya Shirika la Mawasiliano Tanzania mbele ya Kamati ya Bunge ya Miundombinu kilichofanyika kwenye ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni Dodoma.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania Bwana Waziri Waziri Kindamba akifafanua jambo mbele ya Kamati ya Bunge ya Miundombinu kuhusu Muswada wa Sheria ya Shirika la Mawasiliano Tanzania kwenye kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni Dodoma
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: