Mgeni rasmi Philip Alfred Magani kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB Tanzania, Dkt. Charles Kimei akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Shule ya Sekondari Shinyanga na mahafali ya 51 ya kidato cha nne mwaka huu katika shule hiyo.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,mheshimiwa Zainab Telack akizungumza katika maadhimisho hayo ambapo aliwataka wanafunzi kuzingatia masomo yao shuleni na kutumia vizuri mitandao ya kijamii badala ya kuangalia vitu visivyowasaidia katika masomo yao. 
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,mheshimiwa Zainab Telack akizungumza katika maadhimisho hayo ya miaka 50 ya shule ya sekondari Shinyanga na mahafali ya 51 ya kidato cha nne katika shule hiyo. 
Awali Vijana wa skauti wakicheza mchezo wa kutembelea kwa kutumia kamba juu ya mti wakati wa Jubilee ya miaka 50 ya Shule ya Sekondari Shinyanga 'Shy Bush' na mahafali ya kidato cha nne mwaka 2017.Jengo kwa ajili ya watumishi wa shule ya sekondari Shinyanga linaloendelea kujengwa ambalo limewekewa jiwe la msingi leo
Mkuu wa Shule ya Sekondari Shinyanga,Deusdedith Malelemba akitoa maelezo kwa Mgeni rasmi Philip Alfred Magani kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB Tanzania,Dkt. Charles Kimei kuhusu ujenzi wa nyumba za watumishi katika shule hiyo
Mgeni rasmi Philip Alfred Magani kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB Tanzania,Dkt. Charles Kimei akiweka jiwe la msingi katika moja ya majengo yanayoendelea kujengwa katika shule hiyo.

Mgeni rasmi Philip Alfred Magani kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB Tanzania,Dkt. Charles Kimei akipanda mti wa kumbukumbu katika shule ya Sekondari Shinyanga aliyosoma 
Mwalimu mkuu wa kwanza katika shule ya Sekondari Shinyanga, Profesa Geofrey Mmari akipanda mti katika shule hiyo. Profesa Mmari ndiye mwanzilishi wa kampeni ya upandaji miti katika shule hiyo kuzungukwa na msitu.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Zainab Telack akiwasili katika ukumbi palipofanyika Jubilee ya miaka 50 ya Shule ya Sekondari Shinyanga na mahafali ya 51 ya kidato cha nne katika shule hiyo
Meza kuu wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea.Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu Stephen Magoiga,akifuatiwa na Mkuu wa wilaya ya Kishapu,Nyabaganga Talaba,Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack,Mgeni rasmi Philip Alfred Magani kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB Tanzania,Dkt. Charles Kimei na Mkuu wa Shule ya Sekondari Shinyanga,Deusdedith Malelemba.
Wahitimu wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Shinyanga wakiwa ukumbini.
Mwenyekiti wa Bodi ya shule akitoa neno 
Wahitimu wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari Shinyanga wakisoma risala kwa mgeni rasmi 
Wachezaji wa ngoma ya Igembe Sabho kutoka wilayani Kishapu wakitoa burudani wakati wa mahafali hayo 
Mwalimu mkuu wa kwanza katika shule ya Sekondari Shinyanga, Profesa Geofrey Mmari akitoa neno wakati wa Jubilee hiyo ya miaka 50 ya shule ya Sekondari Shinyanga.
Mwalimu mkuu mwingine wa shule ya Sekondari Shinyanga,Zephania Masaki aliyeitumikia shule hiyo kuanzia mwaka 1979 - 1989 akitoa neno 
Wanafunzi wa kidato cha sita katika shule hiyo wakifuatilia kinachoendelea eneo la tukio.
Wanafunzi wa kidato cha tano na sita wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea 
Wanafunzi wakifuatilia matukio 
Wanafunzi waliowahi kusoma katika shule hiyo 
Wanafunzi na walimu waliowahi kufundisha na kusoma katika shule hiyo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: