Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Moita Kiloriti alipokwenda kutembelea mradi wa maji unaohudumia kata hiyo.
Mhandisi Amboka meneja wa TARURA mkoani Arusha akitoa maelezo kwa wananchi namna wakala huo wa barabara za vijijini utakavyotoa huduma katika kata hiyo kwa mwaka huu wa fedha 2017/18.
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amezindua darasa moja katika shule ya sekondari Moita Bwawani,mradi huu umetekelezwa na fedha za 'Lipa kwa matokeo' P4R.

Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ameanza ziara ya siku mbili wilayani Monduli mkoani Arusha. Katika ziara hiyo iliyoanza tarehe 20/10 /2017, alitembelea Kata ya Moita vijiji vya Kilimatinde, Moita Bwawani na Moita Kiloriti, pamoja na kutembelea miradi mbalimbali, kuhamasisha wananchi kujiletea maendeleo na kufanya mikutano ya hadhara katika kila kijiji alichotembelea.

Gambo amehamasisha wananchi wa Kata hiyo kujiletea maendeleo yao wenyewe na akawapongeza kwa kujenga ofisi ya kata kwa nguvu zao wenyewe na akamwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Monduli kupeleka kiasi cha Shilingi Milioni Kumi kumalizia ujenzi huo na akaelekeza jengo hilo liwe limekamilika kabla ya mwezi wa kumi na mbili 2017.

"Kata hii yetu wana Moita na maendeleo yataletwa na sisi wenyewe na sio kumsubiri mzungu atuletee, katika risala yenu mmesema hapo shule ya msingi Kilimatinde kuna upungufu wa darasa moja, tutakwenda kuchanga hapahapa tujenge darasa hilo" alisema Gambo.

Katika harambee ya kuchangua ujenzi wa darasa la shule, Gambo amewachangia wananchi hao bati 60, wanachi wawili wamechanga tofali 2000 kwa kutoa shilingi milioni 4 na chama cha mapinduzi wilaya kimetoa mifuko thelathini kuchangia ujenzi wa darasa hilo.

Ziara hii imezindua darasa moja katika shule ya sekondari Moita Bwawani, darasa lililojengwa kwa mpango wa 'Lipa kwa matokeo (P4R)'.

Mkuu wa mkoa Gambo ameambatana na wataalam kutoka sekta mbalimbali ikiwemo maji, barabara na umeme ambapo kero mbalimbali za wananchi hususan maji ndio iliyoonekana kuwa changamoto katika eneo hilo lakini wataalam wakawakikishia wananchi kwamba serikali inafanyia kazi kilio chao na ndani ya muda mfupi tatizo hilo litakwisha katika sehemu kubwa.

Ziara hii inaendelea leo tarehe 21/10/2017 na Mhe Gambo anatembelea kijiji cha Kipok kuzindua mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi katika shule ya msingi Kipok ambapo atafanya mikutano miwili ya hadhara na kuzungumza na wanachi wa vijiji vya Kipok na Loolera.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: