Na Mwandishi Wetu.

Tamasha la nne linalojumuisha muziki wa kiasili na kimataifa nchini, linalojulikana kwa jina la kigeni kama Karibu Music Festival linatarajia kutimua vumbi Ijumaa hii katika viwanja vya Mwanakalenge Bagamoyo Mkoani Pwani, ambapo vikundi zaidi ya 30 vinatarajiwa kutoa burudani bure kwa Wakazi wa Bagamoyo kwa siku tatu mfululizo.

Mratibu wa Tamasha hilo maarufu duniani Richard Lupia ameiambia Mdimuz Blog kwamba maandalizi ya tamasha hilo lenye lengo la kukutanisha marafiki, kukuza sanaa na utamaduni pamoja na kuitangaza Tanzania nje ya mipaka yake yamekamilika, na tayari makundi kutoka nje ya nchi yatakayohusika na utumbuizaji katika tamasha hilo yameanza safari ya kuja Tanzania.

 Lupia ametaja baadhi tu, ya wasanii kutoka nje ya nchi wanaokuja kushiriki tamasha hilo kuwa ni pamoja na Jackie Paladino kutoka Marekani, De Lukes na Selmor Murtukudzi kutoka Zimbabwe, Total Hp Hop Replacement judoka Denmark, Bernice Boikanyo kutoka Afrika ya kusini, Motra Music na Fadhilee Itulya kutoka Kenya na Nigun Yerushalmy kutoka Izrael.

Pamoja na maonesho ya jukwaani, Yamaha pia litaambatana na semina kwa wasanii wa ndani ambapoembat watakuwa wakiongezewa uelewa juu ya sanaa na utamaduni katika ngazi ya kimataifa na pia hapo hapo uwanjani kutakuwa na maonesho ya kazi za sanaa ya mikono.

Kwa upande wa Tanzania wasanii watakaowakilisha watakuwa ni Laveda, Wamwiduka Band, Safi Theatre, Wahapahapa, GodyKaozya, Jwagwa Music na Dus Top Acoustic.

Bw Lupia amewahakikishia wakazi wa Bagamoyo burudani iliyotawaliwa na usalama wa hali ya juu huku akisisitizwa kwamba vikundi alivyovtaja kushiriki tamasha ni baadhi tu ya vikundi, kuna zaidi ya burudani katika tamasha la mwaka huu. 

Tamasha litaanza Ijumaa ya tare tatu, Novemba na kumalizika Jumapili ya Tarehe tano Novemba mwaka huu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: