Thursday, October 19, 2017

MULTI CHOICE TANZANIA KUADHIMISHA MIAKA 20 YA KUWAPO NCHINI KWA MAONESHO YA BIDHAA ZAKE

Meneja Uhusiano wa Multi Choice Tanzania Johnson Mshana akizungumza na Waandishi.

Kampuni ya MultiChoice Tanzania inayomiliki king’amuzi cha DStv, imesherehekea miaka 20 tangu ianze kutoa huduma nchini jana Jumatano Oktoba 18, 2017.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Meneja Uendeshaji wa kampuni hiyo, Baraka Shelukindo amesema maadhimisho hayo yatajumuisha maonyesho ya siku mbili yatakayofanyika Mlimani City, jijini Dar es Salaam Oktoba 19 na 20.

Amesema DStv ilianza na chaneli tatu za SuperSport, M-Net na Movie Magic na leo inajivunia kuwa na zaidi ya chaneli 100 na redio katika vifurushi vya aina mbalimbali.

Amesema kampuni hiyo imegusa maisha ya mamilioni ya Watanzania ikitengeneza ajira 100 moja kwa moja kwenye kampuni, wafungaji wa DStv wa kujitegemea zaidi ya 1,000 na wauzaji wa moja kwa moja takriban 500.
Meneja Uendeshaji Baraka Shelukindo.
Mkuu wa Channel ya Africa Bongo Magic Barbara Kambogi.
Wanahabari wakisikiliza kwa makini.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu