JPM: Napenda nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa uhai, na mshukuru Mwenyekiti kwa ALAT kwa kunifanya mgeni rasmi, nilitamani kushiriki maana natambua ninyi ndio chachu ya maendeleo kwa sababu munaishi na watu huko

JPM: Nashukuru pia kwa pongezi zake (Mwenyekiti wa ALAT) kwa Serikali ya Awamu hii ya Tano

JPM: Napenda kuwapongeza wewe mwenyekiti, na wote kwa kuchaguliwa kwenu, na napenda kuwahakikishia kuwa Serikali itaendelea kufanya kazi kwa pamoja nanyi. Hii ni fursa nzuri kuzungumza na wananchi hasa ukizingatia ni mara ya kwanza kuhudhuria mkutano huu

JPM: Tangu tumeingia madarakani tumefanya mambo mengi na kwa kushirikiana na ninyi;

JPM: Kwanza mtakumbuka tulianza kuimarisha ukusanyaji mapato kutoka Bil. 850 hadi Tri. 1.3 kwa mwezi

JPM: Tuliamua kudhibiti ubatilifu wa mali za umma, tulidhibiti safari za nje na walsha walsha zimepungua

JPM: Tumeweza kulipa mishahara kwa wakati

JPM: Tunafanya Ujenzi wa Reli ambayo itaweza kubeba mizingo mizito, na Treni ziendazo kwa kasi. Ujenzi wa kipande cha Kilometa 300 Dar – Morogoro umeanza Tri 2.74 na zinatolewa na serikali na juzi tumesaini kipande kingine toka Morogoro - Dodoma

JPM: Pia unafanya upanuzi wa Bandari zetu; Tunafanya upanuzi wa bandari, Mtwara na Dar. Bandari ya Mtwara imegharimu Bil. 134 fedha za Serikali

JPM: July Jiwe la Msingi upanuzi wa bandari ya Dar limewekwa, bandari itaweza kubeba meli kubwa na zenye mizigo mikubwa. upanuzi huu ni kwa sababu mizigo ni mingi bandarini

JPM: Pia tunakarabati viwanja vya ndege mbali mbali nchini; kiwanda cha Julius Nyerere Dar itagharimu Bil. 560 pia viwanja vya Mwanza Bil. 90, kiwanja cha Mtwara Bil. 46, Iringa Bil. 36 na viwanja vingine pia

JPM: Tumenunua Ndege mpya 6; 2 zimewasili na nyingine zitakuja. Moja ina uwezo wa kutoka Marekani hadi hapa bila kusimama kokote. Nchi yenye ndege inafanya vizuri sana kwenye utalii, Watalii wakipitia nchi nyingine wakaona wanyama hawawezi kuja Tanzania

JPM: Tumeshatangaza tenda ya mradi wa Stiegler's gorge utakaozalisha Megawatts 2,100. Makampuni zaidi ya 75 yameomba tenda hiyo

JPM: Kuhusu Umeme kufika Vijijini, Serikali inatarajia kufikisha umeme kwenye vijiji takribani 7873 hadi ifikapo 2020/21

JPM: Pia Barabara kadhaa tumetengeneza za karibu kilometa 1500 za kiwango cha lami. Pia barabara ya Dar - Chalinze itaanza kujengwa hivi karibuni kiwango cha lami kwa njia sita.

JPM: Tazara njia za juu ziaendelea kujengwa. Ubungo ujenzi utaaanza hivi karibuni barabara zitakuwa za ngazi tatu, Ujenzi huu utagharimu Bil. 177.42

JPM: Ujenzi wa BRT utaendelea kwa awamu ya pili, ya tatu na ya nne na utagharimu Bil. 891 kwa ujumla na fedha hizi ni soft loan kutoka benki ya Dunia

JPM: Tumeweza kufuta utitiri wa kodi mbalimbali kwa Wakulima, Wafugaji na Wavuvi. Tumefuta kodi 7 kwa wakulima, KODI 5 kwa Wavuvi na 2 kwa Wafugaji

JPM: Tumefanikiwa kupunguza bei ya mbolea za kupandia na kukuzia kwa kutumia Bulk Procurement System

JPM: Tumeweza kushusha bei ya mbolea mathalani mkoa wa Lindi mbolea ya kupandia na kukuzia imepungua kutoka Tsh. 100,000/= hadi 51,000/=

JPM: Yanayofanyika kwenye migodi ni mambo ya hovyo, hovyo. Kuna document tena zinasainiwa na watanzania kwamba watu fulani wasilipe kodi wala ushuru

JPM: Kule kwenye Tanzanite, Tanzania sio ya kwanza wala ya pili kwenye uuzwaji wa Tanzanite wakati yanachibwa hapa na ndio maana yakaitwa Tanzanite

JPM: Katika uuzwaji wa Tanzanite Duniani kote Tanzania imepata 5% tu na 95% kuliwa na nchi nyingine

JPM: Halafu mnataka nisiseme kwa sababu gani, kisa kuogopa uhai wangu? Mlinichagua wa nini sasa

JPM: Tumekalia Uchumi wetu na sisi viongozi lazima tueleze ukweli. Ndio maana pale tanzanite tumejenga uzio na thamani ya uzio hata hauzidi Bil. 6

JPM: Na ndio maana tulivyozuia kidogo tu, uzalishaji wa Tanzanite umepanda zaidi ya mara 30, siku moja walipata zaidi ya Kilo 18. Haijawai kutokea toka Tanzanite ianze kuchimbwa

JPM: Najua wapo walioumia na mabadiliko haya, kwa kiingereza wanasema "No Sweet Without Sweat" au "No Pain No Gain" ila Watu wengi wanao lalamika hivi sasa ni wale waliokuwa wanategemea mfumo wa zamani

JPM: Palikuwa na Benki moja hapa ilipata hasara ya negative 6, ikaongezewa hela. Ikapata hasara zaidi ikaongezewa hela sasa ikapata hasara ya negative 22. Tumeifunga. Sasa watu kama hawa hawawezi kutupenda na mimi sitaki wanipende ilimradi napendwa na Watanzania

JPM: Watu 12,000 Waliotumbuliwa kwa Vyeti feki hawawezi kunipenda, na hao ndio wanaopiga kelele kwenye mitandao huko. Tanzania ina watu milioni 52 sasa hawa (12,000) hata hawanisumbui nikiwaona 'I Just Enjoy Them'

JPM: Nikizungumza hivi waliokuwa wananufaika hawawezi kunipenda - Sikuja kuuza sura, nikipendwa na Mke wangu inatosha

JPM: Kwenye Halmashauri 140, kulikutwa na pembejeo hewa za Kilimo zenye thamani ya Shilingi Bil. 57.9. Hata Chato kwetu kulikuwa na huu uozo, pembejeo hewa za thamani ya Shilingi Bil. 1.5

JPM: Wanafunzi hewa 65,000 kutoka Elimu ya Msingi mpaka Chuoni. Wanafunzi hewa wanaopokea Mikopo walikuwa 8500.

JPM: Ungekuwa mimi umekuta li-Tanzania liko hivi, uozo kila kona ungefanyaje? Ningekuwa Mhehe ningejinyonga, ningesema "Swela"

JPM: Kuhusu madawa ya kulevya; Watoto wetu wanatokwa na makamasi (uteja wa madawa), wakati watoto wao (wauzaji wa madawa) hawatokwi makamasi

JPM: Mkuu wa Mkoa wa Dar, alijaribu kupambana na watu wa madawa ya kulevya vita ikawa kubwa kwake. Sijui hajasoma sijui nini, Mimi hata kama hajasoma wala nini ilimradi anashika wa madawa ya kulevya huyu ni msomi mzuri. Maana hata hao wasomi wengi wametuangusha. Mimi hata kama hajui 'A' lakini kama anashika madawa ya kulevya huyo ni msomi mzuri

JPM: "nimesikia unakusanya hela, umekusanya shilingi ngapi?" Makonda anajibu kuwa "Milioni 186".

JPM: Sasa kwa nini wakuu wa mikoa wengine hawaigi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar? Waziri Mkuu hebu waambie Wakuu wa Mikoa wengine waige kwa Makonda

JPM: Nimepata taarifa kuwa kuna Wakurugezi wanne watano ni walevi sana, sasa hao lazima wataondoka. Mkurugezi kaa mbali na pombe ukienda huko hata wakuone umebadilika

JPM: Imebainika mara nyingi utekelezaji wa miradi hauendani na pesa zinazotolewa, Tafadhalini zipeni kipaumbele pesa za Serikali. Nchi zinazoendelea wananchi wake hawakwepi KODI, niwahakikishie kuwa kila senti itakayokusanywa itatumika kikamilifu

JPM: Wakati nachaguliwa nilikuta mikoa zaidi ya 22 inasumbuliwa na kipindupindu nikwa najiuliza kwa nini hiki kipindupindu kilikuwa kinanisubiri tu mimi? Nilikuwa naongea na waziri mkuu. Lakini tulipeleka madawa mikoani humo

JPM: Leo ukinambia niongeze posho za Madiwani maana yake nisipeleke Madawa
Hospitalini, maana yake nisipeleke Bilioni 23 kila mwezi za watoto wetu kusoma. Hivyo niwaombe viongozi wetu tufanye kazi, tuwe wavumilivu. Na ndio maana nilipoingia madarakani sikupandisha mishahara na sitapandisha.

JPM: Madiwani unatakiwa uwe na kazi ya kukupatia kipato, unapojaza fomu za kugombea udiwani kuna sehemu unajaza kuwa uwe na kazi ya kukupatia kipato. Sasa kama kuna diwani hana kazi ya kumpatia kipato ajiuzulu

JPM: Kuhusu swala ya Wafanyakazi mwaka jana hatukuajiri wafanyakazi labda sehemu tu muhimu kwa dharura, kwa sababu tulikuwa tunataka kusafisha kwanza, kuwaondoa wenye vyeti feki na Wafanyakazi hewa. Mwaka huu tumetangaza nafasi za kazi, wizara ya afya wametangaza nafasi 3000, Jeshini wametangaza na walimu nadhani wametangaza.

JPM: Sijapandisha mishahara ya watumishi na sitapandisha kwa sababu sikuchaguliwa kupandisha mishahara. Nilichaguliwa kusaidia wananchi wanyonge wapate huduma. Jukumu langu ni kutoa huduma kwa wananchi.!

JPM: "Nimeshasema siongezi mshahara yenu. Kwani tayari nilishawaambia hilo siongezi. Kuna kipengele kinachosema kuwa ukitaka kuwa Diwani ni lazima uwe na kazi nyingine ya kukuingizia kupato. Kwa hiyo kama wewe unaona mshahara huo hautoshi jiuzuru waachie wengine. Maana zipo shughuli nyingi tu za kufanya. Alat Oyee,"

JPM: Niwaombe msiaijiri wenye vyeti feki, hata kama ni ndugu yako atakupa matatizo, bora upokee mshahara wewe ukampe kama unataka aishi vizuri

JPM: Tulipoingia tulikuwa tunalipa mishahara Bilioni 777 lakini tumepunguza mpaka mwezi uliopita tumelipa Bilioni 251. Na wakati huo huo tunalipa deni la Bilioni 950

JPM: Nitafuatilia mazungumzo yenu na nataka mzungumze kwa uwazi kama vile mimi nilivyozungumza kwa uwazi wala hamtanikwaza. Nina matumani pia katika mikutano yenu mambo ya vyama hayatajitokeza maana najua ALAT mnatekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi ya uchaguzi wala hakuna siri, ndio maana katibu mwenezi wa chama huyo hapa hawa ndio wenye ilani

JPM: Kuna taasisi za umma zilikua zinafanyia mikutano ya bodi nje ya nchi. Wakiwa huko wanapandishiana mishahara hadi mil.40. Mimi mshahara wangu ni mil.9 tu kwa mwezi. Sasa nimezuia mikutano ya bodi kufanyika nje. Waliokua wananufaika hawawezi kunipenda. Lakini nikipendwa na mke wangu inatosha, sikuja Ikulu kuuza sura.

JPM: Makamu wa Rais amebakiza miezi miwili tu ahamie Dodoma. Mimi nitahamia mwakani. Halafu nione ambaye atabaki Dar es Salaam. Atanieleza.

JPM: "Nawashukuru Wabunge kupitisha Sheria ya kulinda rasilimali zetu"

JPM: "Vita ya Uchumi ni ngumu kuliko vita ya kawaida"-

JPM: Serikali ya India imetoa mkopo wa masharti nafuu wa USD Mil. 500 za kutekeleza miradi ya maji kwenye miji 17 ikiwemo Zanzibar

JPM: Ukitaka kufanikiwa lazima watakuwepo watakaominywa- Ethiopia wanaongoza kwa ukuaji uchumi lakini wengine wanakimbia
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: