Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akiwaelekeza wakulima wa pamba kijiji cha Msai wilayani Iramba, vipimo vya kati ya tuta na tuta, shimo na shimo kwa kutumia kamba na vijiti ili waweze kupanda kitaalamu na kuvuna kwa wingi.
Wakulima wa pamba kijiji cha Msai wilayani Iramba, wakishiriki kwa vitendo mafunzo yya kupima urefu kati ya tuta na tuta, shimo na shimo kwa kutumia kamba na vijiti ili waweze kupanda kitaalamu na kuvuna kwa wingi.
Katibu Tawala Wilaya ya Iramba Pius Songoma akishiriki kuwaelekea wakulima wa pamba kijiji cha Msai wilayani Iramba, vipimo vya kati ya tuta na tuta, shimo na shimo kwa kutumia kamba na vijiti ili waweze kupanda kitaalamu na kuvuna kwa wingi.
Konyo Mjika ambaye ni mkulima hodari wa pamba wilaya ya Iramba kutoka kijiji cha Msai akimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Singida kwa zawadi ya kilo tano za mbegu ya pamba aliyopewa.
Zakaria Marko Mwakilishi wa Kampuni ya Biosustain itakayosambaza mbegu za pamba tani 300 mkoani Singida akizungumza na wakulima wa zao hilo Katika kijiji cha Msai Wilayani Iramba.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Iramba Emmanuel Luhahula, asimamie kuvunjwa kwa bodi ya Ushirika wa Kijiji cha Msai Wilayani Iramba ndani ya wiki mbili, kutokana na tuhuma za ubadhirifu wa zaidi ya shilingi milioni 50.

Dkt Nchimbi ametoa agizo hilo mwishoni mwa wiki alipokuwa katika mkutano na wakulima wa Pamba wa Kijiji cha Msai, ambao wamemueleza kutokuwa na imani na viongozi wa bodi hiyo kutokana na upotevu wa fedha hizo na wakiwa hawajachukuliwa hatua yoyote.

Wakulima hao wamemueleza Mkuu wa Mkoa kuwa fedha zaidi ya milioni 50 zilitolewa na seikali kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la ghala la ushirika wa kijijini hapo lakini hakukuwa na ujenzi wowote uliofanyika huku wakifuatilia hawapewi majibu sahihi.

Wamesema wana ushirika walijitahidi kutuma mwenyekiti wa Kijiji hicho kufuatilia upotevu huo bila mafanikio jambo lililowakatisha tamaa ya kuendelea na ushirika.

Dkt Nchimbi amesema “moja ya Muhimili wa mafanikio ya kilimo cha pamba ni ushirika ulio imara, tunakoelekea kwenye kilimo cha pamba chenye tija hawa wasiowaaminifu kwenye bodi watatukwaza na kutukwamishwa, kama bodi haifanyi kazi vizuri kwanini iendelee?, Mkuu wa Wilaya naimani kwa utendaji wako mzuri hili halitachukua zaidi ya wiki mbili”.

Aidha amemtaka Afisa Ushirika Mkoa wa Singida kusimamia na kutoa ushauri wa kitaalamu wakati wa kuvunjwa kwa bodi hiyo kwakuwa kazi ya mkoa ni kusuluhisha sio kutafuta maelezo marefu huku wananchi wanapotezewa muda.

“Afisa Ushirika hakikisha tarehe ishirini mwezi huu bodi hiyo iwe imeivunjwe na kuundwa bodi mpya ambayo itasimamia ushirika kwa umakini ili kuinua kilimo cha pamba Iramba”, amesisitiza Dkt Nchimbi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: