Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Juma Kiroboto, maarufu Juma Nature, akisababisha jukwaani, katika Tamasha la 'Gusa Maisha yao' lililofanyika leo kwenye Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo liliandaliwa na Uhuru FM katika kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere.
Mwanamuziki wa muziki Isha Mashauzi akipagawisha mashabiki, katika Tamasha la 'Gusa Maisha yao' lililofanyika leo kweneye Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo liliandaliwa na Uhuru FM katika kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu NyererE.
Mwanamuziki wa muziki wa Singeli Dula Makabila akiwa jukwaani, katika Tamasha la 'Gusa Maisha yao' lililofanyika leo kwenye Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo liliandaliwa na Uhuru FM katika kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere.


Mwanamuziki wa muziki wa Singeli Dula Makabila akiwapandisha mori mashabiki wake walioamua kupanda jukwaani na kuonyesha uhodari wao wa kucheza muziki huo, katika Tamasha la 'Gusa Maisha yao' lililofanyika leo kwenye Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo liliandaliwa na Uhuru FM katika kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere.
Wanamuziki wa bendi ya TOT Plus wakishiriki kunogesha tamasha hilo. Kulia ni kiongozi wao Abdul Misambano.
Mcheza shoo wa TOT Plus Gabriel Romao maarufu kwa jina la Matukutuku akionyesha uwezo wake jukwaani
Matukutuku wa TOT akicheza hadi kwa kichwa chini kukata kiu ya machabiki kwenye tamasha hilo


KatamuTamu wa TOT Plus akionyesha uwezo wake wa kucheza shoo jukwaani.
Mwimbaji mkongwe wa muziki wa Dansi, Anna Mwaole akionyesha bado wamo, wakati akiimba na bdndi hiyo ya Vijana jazz. Anasema yeye ni Kongoro la supu lisiloisha utamu na pia ni kisu cha mgema.
Cosmas Adilian na Mohammed kandera wakionyesha umahili wa kupuliza tarumpeta katika bendi hiyo ya Vijana Jazz.
Mwenge Jazz wakishambulia jukwaa.
Mwimbaji wa Mwenge Jazz akikoleza kwa kusakata muziki jukwaani.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: