Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi (kulia) akizungumza na washiriki (hawapo pichani) wa semina iliyoandaliwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kwa wanahabari juu utabiri mpya msimu wa mvua za Novemba hadi Aprili 2018, wakati akifungua rasmi semina.
Sehemu ya wanahabari wakiwa katika semina iliyoandaliwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)kwa wanahabari juu utabiri mpya msimu wa mvua za Novemba hadi Aprili 2018, unaotarajiwa kutolewa na mamlaka hiyo Oktoba 17, 2017 jijini Dar es Salaam. Utabiri wa msimu wa mvua za Novemba mwaka huu hadi Aprili 2018, kwa maeneo ya kusini mwa Tanzania unatolewa kwa mara ya kwanza mwaka 2017.
---
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa msimu wa mvua unaoanza mwezi Novemba hadi April 2018 kwa maeneo yanayopata Msimu mmoja wa Mvua.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Agnes Kijazi alisema kuwa kwa maeneo hayo yanayopata mvua za msimu mmoja wanatarajia kupata Mvua zilizo juu ya wastani katika maeneo Mangi.

“Mvua hizo zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo ya Dododma, Singida, Kigoma, Tabora, Rukwa, Katavi, Mbeya, Songwe, Morogoro, Itinga, Ruvuma, Lindi na Mtwara ambapo baadhi ya amaeneo hayo Mvua zinatarajiwa kuwa kuanza wiki ya kwanza ya mwezi Novemba” Alisema Dkt Kijazi.

Aidha aliendelea kwa kusema kuwa tahadhari inatakiwa kuchukuliwa na jamii kwa Vipindi vya Mvua kubwa katika maeneo hayo vinataraiwa kuwepo.

“Matukio ya Vipindi vifupi vya Mvua kubwa yanatarajiwa kusabaisha Mafuriko katika Maeneo machache”Alisema Dkt Kijazi.

Hata hivyo aliendelea kwa kusema kuwa Kwa ujumla msimu wa mvua kubwa unatarajia kuanza mwezi January mwaka 2018.

“Msimu huu ni mahususi katika amaenmeo ya magharibi mwa nchi,Kanda ya Kati,Nyanda ya kati,Nyanda ya juu kusini magharibi pamoja na kusini mwa nchi” Alisema Dkt Kijazi.

Hali ya Joto la juu ya wastani iliyopo magharibi mwa Bahari ya hindi inatarajiwa kuendelea kuwepo katika kipindi cha Novemba 2017 hadi April 2018.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: