Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Sinyamule akizungumza wakati akitoa mada kwa Vijana wa Ukwata Wilaya hiyo na kabla ya kuzindua kitabu cha A NOBLE GIRL OF NOWDAYS".
 Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Sinyamule akizungumza wakati akitoa mada kwa Vijana wa Ukwata Wilaya hiyo na kabla ya kuzindua kitabu cha A NOBLE GIRL OF NOWDAYS".
Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Sinyamule akizindua kitabu cha A NOBLE GIRL OF NOWDAYS".
Wanafunzi wa UKWATA wamsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Same juu ya mada ya Uzalendo

Na Mwandishi Wetu.

Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Senyamule amewataka Vijana kuwa wazalendo hili kuweza kuyaenzi yale yote yaliyofanywa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika kipindi cha uhai wake .

hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Sinyamule alipokuwa akitoa mada kwa vijana iliyohusu "Kijana na Uzalendo" kwa Vijana wa Ukwata zaidi ya 1000 wa Wilaya ya Same na uzinduzi wa Kitabu kilichohusu Maisha ya Mwalimu Nyerere.

"Mwl. Nyerere alivyokuwa mzalendo na mpaka sasa ndiye Mtanzania wa kwanza aliyeonyesha Uzalendo wa kiwango cha juu kabisa akifuatiwa na Rais wetu wa sasa Mh. Dr. John Pombe Joseph Magufuli hivyo nyie Vijana Mnapaswa kuenenda kama viongozi wetu hawa wanavyotutaka hili tuwe na Taifa la Wachapakazi na Wazalendo" amesema Sinyamule.


katika Uzinduzi wa kitabu kilichoandikwa na Kijana kwa ajili ya kuelimusha vijana wa kike kujitambua na kuchukua hatua muhimu kwa ajili ya mustakabali wao wa baadaye kinachokwenda kwa jina la " A NOBLE GIRL OF NOWDAYS".


Mara baada ya kuzindua kitabu hicho mkuu wa Wilaya hiyo aliweza kununua vitabu 51 na kuagizwa visambazwe kwenye shule zote 51 za Sekondari Wilaya ya Same, viwekwe maktaba ili wanafunzi waweze kuvisoma

Aidha Dc Sinyamule alimpongeza mwandishi wa kitabu hicho Elihuruma kwa uandishi huo na kumtaka aendelee kuandika vitabu vingi zaidi kwa faida ya Vijana na watanzania kwa ujumla.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: