Balozi wa Tanzania nchini China akijadiliana jambo na aliyekuwa Balozi wa China nchini Tanzania Lu Youqing walipokutana jijini Guangzhou katika mkutano wa wafanyabiashara wa Tanzania na wale wa China kujadili fursa mbalimbali za biashara na uwekezaji.
Aliyekuwa Balozi wa China nchini Tanzania, Balozi Dk. Lu Youqing akiongea katika majadiliano ya kibiashara baina ya wafanyabiashara wa Tanzania na China ambayo yalienda sanjari na maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Canton jijini Guangzhou, China.
Baadhi ya wafanyabiashara kutoka Tanzania akifuatilia mada katika mkutano wa kujadili fursa mbalimbali za biashara na uwekezaji baina ya wafanyabiashara wa Tanzania na wale wa China wakati wa maonesho ya Kimataifa ya Bisashara ya Canton yaliyomalizika hivi karibuni jijini Guangzhou, China. (Picha zote na Rodney Thadeus - MAELEZO).

NA RODNEY THADEUS, CHINA.

Rais wa Tanzania Dk. John Magufuli amekuwa gumzo hapa nchini China kutokana na Serikali yake kuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi.

Aliyekuwa Balozi wa China nchini Tanzania Lu Youqing na baadhi ya wafanyabiashara wakubwa wa China ambao wanataka kuwekeza nchini Tanzania, wamemuelezea Rais Magufuli kama kiongozi aliyeonyesha utashi na ushujaa wa hali ya juu kupambana na rushwa ambayo imekuwa ni tatizo kubwa miongoni mwanchi za Afrika.

Rais Magufuli alielezewa katika majadiliano maalum yaliyoandaliwa kuwakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania na China kujadili fursa za kibiashara, ikiwa ni sehemu ya Maonesho ya Kimataifa ya Canton yaliyofanyika katika jiji la Guangzhou nchini China.

“Tangu Rais Magufuli aingie madarakani kuna mambo makubwa yamefanyika katika mapambano dhidi ya rushwa. Serikaliya China itaendelea kuunga mkono juhudiza Rais Magufuli kupambana na rushwa,” alieleza Balozi Lu Youqing.

Balozi Lu lieleza wazi kwamba msimamo wa Rais Magufuli wa kutovumilia vitendo vya rushwa, utajenga misingi imara ambayo itasaidiaTanzania kutimiza malengo yake ya kuwa nchi ya uchumi wa kati wa viwanda ifikapo mwaka 2025.

Pamoja na kusifu juhudi zinazofanywa na Serikali kudhibiti rushwa nchini Tanzania, Balozi Lu amewaeleza wafanyabiashara wa China wanaotaka kuwekeza nchini kuwa Tanzania ni nchi yenye mazingira bora a uwekezaji kutokana na uimara waukuaji wa uchumi ambao umekuwa ukikua kwa zaidi ya asilimia saba kwa mwaka na kuwa nchi inayoongoza kwa ukuaji wa uchumi Afrika Mashariki.

“Tanzania ni nchi yenye amani na utulivu wa kisiasa na kuleta matumaini katika uwekezaji. Napenda kuwashauri wafanayabiashara na makampuni yanayowekeza Tanzania kumuunga mkono Rais katika vita yarushwa,” alieleza Balozi Lu uku akisisitiza kuendelezwa kwa ushirikiano uliopo kati ya nchi hizo mbili.

Pia katika mkutano huo, Makamu wa Rais Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo wa China kwa nchi za Afrika (CADFund) ambao unasaidia makampuni kuwekeza Afrika, Wang Yong alieleza kuwa Tanzania ninchi muhimu kwa uwekezaji miongoni mwanchi za Afrika hasa katika kilimo, madini na nishati.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: