Mkuu wa tawi la benki ya NIC lililopo Kariakoo, Majid Mohamed akiongea na wanawake wajasiriamali (hawapo pichani) waliofika katika tawi hilo kwaajili ya kukabidhiwa zawadi ikiwa ni ishara ya benki hio kutoa shukrani kwa wateja wake huku ikiadhimisha wiki ya huduma kwa wateja.
Meneja wa idara ya Wateja wadogo na taasisi wa benki ya NIC, Natasha Cathles akiwashukuru wanawake wajasiriamali pamoja na wateja wengine kwa kuwa wateja wao na hatimaye kutoa zawadi kwa Wanawake wajasiriamali hao ikiwa ni ishara ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja
Mmoja wa wateja na mwanamke mjasiriamali wa Kariakoo, Bi Lucia Mlimi akiwashukuru wafanyakazi wa benki ya NIC tawi la Kariakoo na uongozi kwa ujumla kwa kuona mchango wao na kuamua kuwatunuku zawadi mapema leo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja
Wanawake wajasiriamali wakipokea zawadi zao mapema leo
Zawadi zikiendelea kutolewa kwa wanawake wajasiriamali hao
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya NIC wakiwa katika picha ya pamoja na wanawake wajasiriamali wa Kariakoo ambao wamepewa zawadi na benki hio ikiwa ni ishara ya kutoa shukrani kwa wateja wao na kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja
Wanawake wajasiriamali wa Kariakoo pamoja na mfanyakazi wa benki ya NIC wakikata keki kuashiria maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja na kufurahi pamoja na wanawake hao kwa kuwapa zawadi
Baadhi ya wanawake wajasiriamali waliopokea zawadi kutoka Benki ya Nic mapema leo. Picha Zote na Josephat Lukaza | Lukaza Blog.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: