Washiriki wa shindano la kutafuta mrembo wa mkoa wa Shinyanga “Miss Shinyanga 2017”,wameunga mkono kampeni ya upandaji miti iliyoanzishwa katika wilaya ya Shinyanga na Mkuu wa wilaya hiyo Josephine Matiro hivi karibuni ili kupambana na hali ya ukame/jangwa mkoani humo. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog.
Washiriki wa shindano la Miss Shinyanga 2017 wakitoka Diamond Fields Hotel walipoweka kambi mjini Shinyanga wakielekea kwenye maeneo ambayo yamepandwa kwa ajili ya kuweka maji kwenye miti hiyo.Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Washiriki wa shindano la kutafuta mrembo wa mkoa wa Shinyanga “Miss Shinyanga 2017” wakiwa wamebeba madumu ya maji kwa ajili ya kuweka kwenye miti ambayo inamwagiliwa maji kwa njia ya makopo ya maji yaliyotobolewa kwa ajili ya kutoa matone kidogo kidogo.
Mshiriki wa shindano la Miss Shinyanga 2017 akimwaga maji kwenye kopo jingine.
Mrembo akimwagia maji mti kwa kuweka maji kwenye kopo lililowekwa kwenye mti.
Zoezi la kumwagilia maji miti likiendelea.
Mrembo akimwagilia mti.

Mapema leo Ijumaa Oktoba 13,washiriki hao wa shindano hilo la mrembo wa mkoa wa Shinyanga linalotarajiwa kufanyika Oktoba 15 mwaka huu,walimwagilia maji miti mbalimbali iliyopandwa mjini Shinyanga.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo,Mwandaaji wa shindano la Miss Shinyanga mwaka 2017,Grace Shija alisema pamoja na kufanya maandalizi ya shindano hilo pia wanashiriki katika shughuli za kijamii.

“Sisi kama sehemu ya jamii tumeamua kushiriki katika kampeni ya upandaji miti kwa kumwagilia maji miti iliyopandwa katika maeneo mbalimbali mjini Shinyanga kwa kujaza maji kwenye chupa zilizowekwa kutiririsha matone ya maji kwenye miti hiyo”,alieleza Shija.

Akizungumzia kuhusu shindano la Miss Shinyanga mwaka huu alisema jumla ya warembo 12 kutoka wilaya zote za mkoa wa Shinyanga watachuana siku ya Jumapili Oktoba 15,2017 katika ukumbi wa NSSF ya Zamani mjini Shinyanga kuanzia saa mbili usiku ili kupata mrembo wa mkoa mwaka huu.

Aliwataja wadhamini katika shindano hilo kuwa ni TBL, Shujaa Gin & Vodka, Butiama Club, Diamond Fields Hotel na Lulekia Sound and Decoration.

Nimekuwekea picha hapa chini wakati washiriki wa shindano la Miss Shinyanga wakishiriki zoezi la kumwagilia maji katika miti iliyopandwa hivi karibuni mjini Shinyanga.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: