Miaka 71 ya Ndoa ya Mzee Sylvester Lubala na Mkewe Cecilia Lubala.
Katibu wa Chama cha Mashujaa waliopigana Vita kuu ya pili ya Dunia 1938 hadi 1945 ambaye ni Baba Mzazi wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabulla, Mzee Sylvester Lubala na Mkewe Cecilia Lubala wametimiza Miaka 71 ya ndoa yao iliyofungwa mwaka 1946.

Hafla ya kuadhimisha miaka 71 ya ndoa hiyo imefanyika katika hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam na kuhudhuliwa na watu maarufu pamoja na Viongozi mabilmbali wa kitaifa wakiwemo Mawaziri na Wabunge wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mzee Sylvester Lubala akiwa na Mkewe Cecilia Lubala wakipunga mkono kwa wageni waalikwa wakati wa hafla yao ya kutimiza Miaka 71 ya ndoa iliyofanyika katika hoteli ya Srena Jijini Dar es Salaam na kuhudhuliwa na watu maarufu na Viongozi wa kitaifa.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na MaeNdeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiwa na Mkewe wakitoa pongezi kwa Mzee Sylvester Lubala mara baada ya kutimiza miaka 71 ya ndoa yao.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimpongeza Mzee Sylvester Lubala kutimiza miaka 71 ya ndoa na Mkewe Cecilia Lubala.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Suzan Kolimba wakitoa pongezi kwa Mzee Sylvester Lubala kutimiza miaka 71 ya ndoa na Mkewe Cecilia Lubala.
Baadhi ya Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakitoa pongezi kwa Mzee Sylvester Lubala kutimiza miaka 71 ya ndoa na Mkewe Cecilia Lubala.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni , Ally Api akigonga glasi na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabulla wakati wa hafla hiyo.
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadick na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi na viongozi wengine wakitoa pongezi kwa Mzee Sylvester Lubala kutimiza miaka 71 ya ndoa na Mkewe Cecilia Lubala.
Watoto 18 wa Mzee Sylvester Lubala na Mkewe Cecilia Lubala wakati wa hafla ya miaka 71 ya ndoa yao.
Baadhi ya Wajukuu na Vitukuu wa Mzee Sylvester Lubala na Mkewe Cecilia Lubala wakati wa hafla ya miaka 71 ya ndoa yao.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabulla akihojiwa na waandaaji wa Kipindi cha Chereko kinachorushwa na TBC1
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: