Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.

Baada ya kupita miaka mitano tangu kutokea kwa kifo cha msanii marufu nchini, marehemu Steven Kanumba, Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam, Novemba 13 mwaka huu inatarajia kutoa hukumu dhidi ya kesi ya mauaji ya bila kukusu inayomkabili msanii maarufu wa filamu nchini, Elizabeth Michael 'Lulu'.

Hatua hiyo imekuja baada ya Wazee wa Baraza kutoa ushauri wao kwa mahakamani hapo na kudai kwamba Lulu ameua bila kukusudia.

Katika kesi hiyo, Lulu anakabiliwa na tuhuma za kumuua bila kukusudia, msanii mwenzake marehemu Steven Kanumba, Aprili 7 mwaka 2012.

Mapema kabla ya wazee hao wa Baraza kutoa maoni yao Jaji Sam Rumanyika anayesikiliza kesi hiyo alisoma maelezo ya mashahidi wa pande zote mbili kisha kusikiliza maoni hayo.

Kabla ya kutolewa maoni hayo, Jaji Rumanyika alisema kimsingi ushahidi wa upande wa mashtaka umejikita kwenye ushahidi wa kimazingira kwa sababu mshtakiwa Lulu ndiye alikuwa mtu wa mwisho kuwa na Kanumba.

Jaji Rumanyika amesema kuwa ushahidi wa kimazingira sio wa moja kwa moja lakini kama ungekuwa mnyololo basi vipande vyake vikiunganishwa havikatiki.

Aliwaambia wazee hao wa baraza katika kutoa maoni yao waone kuwa mshtakiwa ndiye alikuwa mtu wa mwisho kuwa na marehemu na vile vile ametoa maelezo ya kina yaliyotosheleza juu ya tukio hilo

Pia alisema, kama wataona mshtakiwa hausiki na mauaji yale wasisite kuieleza mahakama,

"Kama mtaona kifo cha Kanumba kilitokana na ugomvi basi waeleze 

`Aliwaambia katika mashauri ya mauaji siyo lazima upande wa mashtaka kuthibitisha nia ovu bali kutokea, kwa tukio ithibitike kuwa tendo limetendeka.

"Katika maoni mkumbuke msingi wa sheria wa mashtaka ya mauaji ya bila kukusudia kuthibitishwa kwa nia ya mauaji siyo lazima, mara nyingi mauaji ya bila kukusudia yanasababishwa na ugomvi", amesema Jaji.

" Kama mtaona kifo cha Kanumba kilitokana na ugomvi mtoe maoni yenu na kama mshtakiwa hausiki na tukio hili mtoe pia maoni yenu.

Katika maoni yake, Mzee wa Baraza Omary Panzi amesema Lulu kutokana na ushahidi uliotolewa imeonyesha wazi kuwa Lulu ameua bila kukusudia.

Amedai ametoa maoni yake kutokana na ushahidi wa Seth Bosco, mdogo wake Kanumba ambaye alidai ugomvi uliotokea baina ya Lulu na marehemu kaka yake Kanumba.

Mzee wa baraza, Sarah katika maoni yake amedai Kanumba alikufa kutokana na ugomvi ambapo ushahidi pia umetueleza kulikuwa na Giza hivyo Lulu hakuuwa kwa makusudi bali aliuwa bila kukusudia,

Mzee wa baraza wa Tatu, Rajabu Mlawa alidai Kanumba alikufa kutokana na ugomvi baina yao kwa kuwa ndani kulikuwa na ugomvi.

"Elizabeth hakuua kwa makusudi, aliua bila kukusudi, kutokana na sababu ulizosoma sina ubishi,juu ya ushahidi uliotolewa na panda zote mbili, Lulu ameua bila kukusudi ukizingatia Kanumba alikuwa na mwili mkubwa, mnene, mzito mwenye nguvu za kutosha, Lulu hana nguvu, atika hekaheka za kujinusuru maana tumesikia kuwa kulikuwa na kupigwa, pengine Lulu alijitetea kwa nguvu zake chache inawezekana alimsukuma Kanumba akaenda kudondokea ukuta na kupata madhara, kwa maoni yangu kosa la kuua bila kukusudia limethibitika".

Kufuatia hayo, kesi hiyo inatarajiwa kutolewa hukumu November 13 mwaka huu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: