Mgeni Rasmi Bw. Charles Washoma ambaye ni Meneja Mkazi wa Africa Practice mshauri  akitoa shukurani zake za dhati kwa Kampuni ya Bima ya Resolution kwa kuwakutanisha Madalali wa Bima 'Insurance Brokers' toka sehemu tofauti nchini ambapo kwa kufanya hivyo itaongeza zaidi ufanisi na ushirikiano baina yao na Kampuni ya Bima ya Resolution.

Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Resolution na Kampuni ya Mikopo ya 
Resolution Bw. Peter Nduati akielezea mambo mbalimbali kuhusiana na kampuni hiyo na kuwashukuru madalali wa Bima kwa kwa kuungana nao katika chakula cha usiku, pamoja na hayo alisema kuwa wapo Kenya, Uganda na Tanzania, kwa Tanzania wapo Dar es salaam na Arusha lakini hivi karibuni watafika Zanzibar na Mwanza.Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Bima ya  Resolution  Tanzania Bi. 
Maryanne Mugo akieleza kwa ufupi kuhusiana na tukio hilo la kurudisha shukurani, ambapo pia alizitaja baadhi ya huduma wanazozitoa ikiwa nipamoja na; Travel Plan, Medical plan, Liability plan,Home Insurance,Marine insurance na Motor Private Insurance 

Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Bima ya  Resolution  Tanzania Bi. 
Maryanne Mugo (aliye simama nyuma) akiwatambulisha viongozi wa Idara mbalimbali katika kampuni ya Bima ya Resolution wa nchini Tanzania.
Bwana Melkizedech Nyau ambaye ni mtakwimu wa Bima kutoka kampuni ya Bima ya Resolution akielezea bima ya Afya Bora kwa ajili ya watu wenye kipato cha chini kuanzia mwaka 0 hadi 64 ambao ni kama Bodaboda, Mama ntilie,wauza maandazi pamoja na makundi mbalimbali yanayofanana na hayo. Alieleza kuwa ili kujiunga na Bima hiyo itakuwa vizuri watu wawe katika kundi au Vikoba waweze kupata kwa pamoja huduma hiyo bora kutoka kampuni ya Resolution.
Muwezeshaji wa hafra hiyo Bw. Evance Bukuku ambaye pia ni Mchekeshaji maarufu hapa Nchini Tanzania akiendelea kutoa taratibu mbalimbali wakati wa  chakula cha usiku kilicho andaliwa na Shirika la Bima la Resulution katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es salaam.

Muwezeshaji wa hafra hiyo Bw. Evance Bukuku akiwauliza maswali mbalimbali kuhusiana na bima.
Bi. Mailda William(Kushoto) kutoka Aste Insurance Brokers ambao walishinda katika bahati nasibu kutoka Kampuni ya Bima ya Resolution ambapo kiasi cha fedha Tsh 500,000 zitaenda kwa asasi ya kiraia ya Msichana ikiwa ni kurudisha Shukurani kwa jamii kutoka kampuni ya bima ya Resolution


Bi. Jenifa Projest (Kulia) kutoka Aste Insurance Brokers akipewa mkono wa pongezi kutoka kwa mgeni Rasmi Bw. Charles Washoma baada ya  kushinda 
katika bahati nasibu kutoka Kampuni ya Bima ya Resolution ambapo kiasi 
cha fedha Tsh 500,000 zitaenda kwa asasi ya kiraia ya Salvation Army  ikiwa ni 
kurudisha Shukurani kwa jamii kutoka kampuni ya bima ya Resolution

 Bi. Fauzia Bairu (Kulia) kutoka Pioneer Insurance Brokers akipewa mkono wa pongezi kutoka kwa Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Resolution na Kampuni ya Mikopo ya 
Resolution Bw. Peter Nduati baada ya  kushinda 
katika bahati nasibu kutoka Kampuni ya Bima ya Resolution ambapo kiasi 
cha fedha Tsh 500,000 zitaenda kwa asasi ya kiraia ya Sustainable Education ikiwa ni 
kurudisha Shukurani kwa jamii kutoka kampuni ya bima ya Resolution.
 Bw. Emmanuel Mkindi, Meneja wa Maendeleo ya Biashara- Biashara kwa ujumla kutoka Kampuni ya Bima ya Resolution akitoa neno la shukurani kwa madalali wote wa bima waliofika katika tukio lao la 'Appreciation Dinner' ambapo kaulimbiu yao inasema 'Protecting what you value' yani tunalinda unachokithamini.
Madalali wa Bima wakiwa katika hafra ya chakula cha usiku iliyo andaliwa na Kampuni ya Bima ya Resolution kwa ajili ya kurudisha shukurani kwa jamii.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: