Thursday, November 30, 2017

MADABA YAWA MFANO BORA KATIKA KUTATUA KERO YA MAJI KATIKA WILAYA YAO

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akikagua mabomba yatakayotumika kusambazia maji kwa mradi wa Maweso akiwa na Mbunge wa Jimbo la Madaba, Joseph Mhagama katika Wilaya ya Madaba, mkoani Ruvuma.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akikagua ujenzi wa tenki la maji la mradi wa Lolindo na Mbunge wa Jimbo la Madaba, Joseph Mhagama ambao utekelezaji wake unaendelea katika Wilaya ya Madaba, mkoani Ruvuma.
Mhandisi wa Mkoa wa Ruvuma, Jones Kimaro (kulia) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso katika kitekeo cha maji ikiwa ni sehemu ya mradi wa Lilondo katika Wilaya ya Madaba, mkoani Ruvuma.
Mradi wa mfano uliotekelezwa na wakazi wa Lilondo, ambao wametumia teknolojia ya kienyeji ya kukusanya maji kwa mabomba kutoka milimani na kuyahifadhi kwenye bwawa walilochimba na kuyasambaza kwa wananchi kupitia mitaro waliyochimba kwa gharama zao wenyewe ili kukabiliana na changamoto ya maji katika kijiji chao.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu