Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan akimjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Antiphas Lissu aliyelazwa katika hospitali ya Aga Khan jijini Nairobi. Mhe Samia Suluhu Hassan amekwenda kumjulia hali Mhe. Lissu  baada ya kutoka katika sherehe ya kuapishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya kwa awamu ya pili,  sherehe zilizofanyika leo kwenye uwanja wa Moi Kasarani Mjini Nairobi, Kenya. Mhe. Samia Suluhu Hassan amehudhulia sherehe hizo akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: