UBALOZI WA China nchini kwa kushirikiana na Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) pamoja na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) wamezindua uandaji wa filamu maalumu inayolenga vivutio vya utalii, vilivyomo nchini kupitia Reli ya Tazara.

Akizungumza Jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa filamu inayowahusisha wataalam mahiri katika uandaaji wa filamu Duniani, Balozi mdogo wa China hapa nchini Gou Haodong, alisema mbali na kutangaza utalii, filamu hiyo imelenga kuitangaza Reli ya Tazara, iliyojengwa kwa ushirikiano wa nchi ya china Mwaka 1970.

“Alisema pia kutokana na reli hiyo kupitia maeneo mbalimbali ikiwemo hifadhi ya wanyama ya Selous, filamu hiyo itaweza kuwavutia wageni mbalimbali, wakiwemo raia wa china na hivyo kuja kutembelea hifadhi hiyo kupitia reli ya Tazara na hivyo kuliingizia taifa mapato” alisema

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TAZARA Bruno Ching’andu, alisema kutengenezwa kwa filamu hiyo kutakuwa kichocheo kikubwa kwa mamlaka hiyo, hususani kuongeza idadi ya watalii watakaokuja na kusafiri na treni yao kwa ajili ya kujionea vivutio mbalimbali.

Naye Msemaji Mkuu kutoka Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Geofrey Tengeneza, alisema Bodi imevutiwa na mpango wa utengenezaji wa filamu hiyo kwa kuwa utaweza kuwavutia watalii wengi kuja nchini kwa ajili ya kujionea vivuti vilivyopo na hasa hifadhi ya Selous, inapopita reli hiyo.

Alisema kwa kipindi kirefu Serikali ilikuwa na mkakati wake wa kupata watalii wengi kutoka nchi za Asia, na kwamba ujio wa filamu hiyo utasaidia kuongeza kasi ya watalii hao kuja nchini na hivyo kuliingizia Taifa fedha za kigeni.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: