Thursday, December 21, 2017

IDARA YA HABARI MAELEZO YAPOKEA MSAADA WA VIFAA KUTOKA UBALOZI WA CHINA

Waziri wa Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akipokea zawadi ya Krismasi kutoka kwa Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China hapa nchini Mhe. WANG Ke mara baada ya hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa kwa ajili ya Idara ya Habari (MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam. Msaada huo unajumuisha Kompyuta mpakato na samani za ofisi.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akipokea zawadi ya Krismasi kutoka kwa Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China hapa nchini Mhe. WANG Ke mara baada ya hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa kwa ajili ya Idara yake leo Jijini Dar es Salaam. Msaada huo unajumuisha Kompyuta mpakato na samani za ofisi.
Waziri Mshauri wa Ubalozi wa China hapa nchini Gou Haodong akifafanua jambo mbele ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (wa pili kutoka kushoto) walipokutana katika hafla fupi ya makabidhiano ya msaada wa vifaa kwa ajili ya Idara ya Habari (MAELEZO) iliyofanyika katika Ofisi za Ubalozi wa China Jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China hapa nchini Mhe. WANG Ke. Msaada huo unajumuisha Kompyuta mpakato na samani za ofisi. (Picha na: Frank Shija – MAELEZO).

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu