Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya mipango ya matumizi ya Ardhi(NLUPC) Dkt. Stephen Nindi akifungua mkutano wa kikosi kazi kwa ajili ya mchakato wa uanzishwaji wa kanzidata ya mipango ya matumizi ya ardhi,Mjini Morogoro
Mwenyekiti wa Kikao Bw. Jamboi Baramayegu kutoka ujamaa Community akielezea utaratibu wa namna kazi itakavyofanyika
Afisa Tehama kutoka wakala wa Serikali Mtandao Bw. Thomas Malinga akitoa maelezo ya malengo ya wao kushiriki katika mchakato wa uanzishwaji wa uanzishwaji wa kanzi data ya mipango na matumizi ya ardhi.
Afisa Mipango wa Tume ya Taifa ya mipango ya matumizi ya Ardhi Bw. Gelard Mwakipesile, akielezea kwa kina kwa wajumbe wa mkutano kuhusu mipango ya matumizi ya ardhi,mchakato ulipo anzia hadi kuanza kwa mchakato wa uanzishwaji wa kanzi data ya mipango ya matumizi ya ardhi.
Bw. Paulo Tarimo kutoka Wizara ya Kilimo akichangia jambo wakati wa kikao cha mchakato wa uanzishwaji wa kanzi data ya mipango ya matumizi ya ardhi.
Baadhi ya wanakikosi kazi kutoka sekta mbalimbali wakiendelea na majadiliano ya kutoa maoni yao juu ya kuandaa mchakato wa uanzishwaji wa kanzi data ya mipango ya matumizi ya ardhi.
Katibu Mkuu wa Chama cha wafugaji Tanzania Bw. Magembe Makoye akiwasilisha mapendekezo yao kwa ajili ya mchakato wa uanzishwaji wa kanzi data ya mipango ya matumizi ya ardhi kutoka katika kundi la wafugaji
Bw. Godfrey Massay Meneja utetezi kutoka LANDESA akiwasilisha mapendekezo yao kwa ajili ya mchakato wa uanzishwaji wa kanzi data ya mipango ya matumizi ya ardhi kutoka katika kundi la Kilimo.
Afisa Sheria kutoka NLUPC Bi. Devotha Selukele akichangia jambo wakati makundi mbalimbali wakiwasilisha maoni yao juu ya kanzi data
Afisa programu kutoka Haki Ardhi Bw. Joseph Kiombola akiwasilisha mapendekezo yao kwa ajili ya mchakato wa uanzishwaji wa kanzi data ya mipango ya matumizi ya ardhi kutoka katika kundi la Asasi za Kiraia.
Afisa wanyama pori (TAWA) Bw. Herman Nyanda akiwasilisha mapendekezo yao kwa ajili ya mchakato wa uanzishwaji wa kanzi data ya mipango ya matumizi ya ardhi kutoka katika kundi la Maliasili
Afisa Mpelembaji kutoka TNRF Bw. Wilbard akiwasilisha mapendekezo yao kwa ajili ya mchakato wa uanzishwaji wa kanzi data ya
mipango ya matumizi ya ardhi kutoka katika kundi la Utafiti
Wadau wakiendelea na mkutano huo.

Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) ipo mbioni kuanzisha Kanzidata (Database) ya mipango ya matumizi ya ardhi iliyofanyika nchini na wadau mbalimbali wa sekta ya ardhi.

Kwa kushirikiana na wadau wa upangaji, usimamizi na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi wa taasisi za serikali pamoja na asasi za kiraia, Kanzidata hiyo itabeba taarifa zitakazoonyesha maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli mbalimbali kama vile kilimo, malisho, huduma za jamiii, n.k itarahisisha utendaji kazi kwa Tume, mamlaka zingine za upangaji, wadau pamoja na wananchi
kwa ujumla ambao watatumia teknolojia kujua maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli mbalimbali nchi nzima.

Picha na Fredy Njeje/Blogs za Mikoa Tanzania.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: