Inawezekana ukatofautiana na JPM kwa rangi ya chama chake au usukuma wake, Lakini mimi kama mtu tena mtanzania mwananchi mwandamizi nisiye na shaka na uzalendo wangu, Moja ya dhana ambayo tunaweza tukaibeba kutoka kwa Rais Dkt. Magufuli ni dhana ya msisitizo wa kufanya kazi kwa bidii (HAPA KAZI TU).

Dhana hii imebeba ukombozi wa mtu binafasi bila kujali itikadi yake hata kama unatofautiana na Rais au serikali lakini moja ya jambo ambalo linaweza kuwa ukombozi mkubwa ni sisi watanzania kuchukua kwa umakini hii dhana ya kufanya kazi kwa bidii itatusaidia kwa mtu mmoja mmoja, itatusaidia kwa kaya, itasaidia kwa uchumi wa taifa kwa ujumla.

Bado tunatatizo kubwa la kufanya kazi kwa bidii, wapo ambao wameanza kuelewa na wanafanya kazi kwa bidii sana sana, lakini wengi wetu wakiwamo vijana wenzangu bado dhana hii hatujaielewa.

Kwa moyo wa kupenda nawakumbusha na mnielewe kwa umakini kufanya kazi kwa bidiii ndio nguzo ya ukombozi wa mtu kuondokana na umasikini, Vyuma vimekaza lakini njia rahisi sana ni kufanya kazi kwa bidii hamna namna nyingine, Tanzania ni nchi iliyobarikiwa sana sana kwenye sekta moja tu ya kilimo unaweza kufanya kazi kwa bidii kubwa ndani ya miaka miwili na wewe ni milionea sanaa.

Wote tukifanya kazi kwa bidii itatuwia urahisi kupaza sauti ka serikali kufanya marekebisho kwenye huduma za msingi na mazingira tunayoyaona ni tatizo kwenye ufanyajai kazi wetu kwa bidii.

Tutofautiane na JPM kwa rangi ya chama chake ama usukuma wake lakini hili la kufanya kazi kwa bidii analolisisitiza litatusaidia binafsi na litasaidia kwa pamoja hakuna kitu kigumu kama kuongoza taifa la wavivu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: