1. Mnadharau sana kwa Media za Mikoani... Hamjui kuwa nazo zina power kubwa... Katika Ukanda zinakopatikana.... Na huko ndiko Show zinakopatikana... Mtaendelea kulaumu na kumtafuta mchawi nani ikiwa nyie wenyewe ndio mnaojiloga... Mtabaki kulalamika @diamondplatnumz anapendelewa na si vinginevyo... Linapokuja suala la kuachia ngoma huwa anajishusha nakutoa ushirikiano kwa media zote hana dharau.

2. Wasanii wa Dizaini yenu huwa hamfaniki/kusogea nakubaki vilevile au kusafiria nyota za kaka zenu au wasanii wanaowasimamia... Wapo wengi wenye vijitabia hivyo.... Leo namtolea Mfano mtu kama ABDUKIBA ni miongoni mwa wasanii ambao katika suala hilo linawahusu moja kwa moja... Usitegemee Power ya Kaka ako @officialalikiba kuwa muda wote itakuwa msaada kwako... Tambua yeye tayari anamashabiki wake really ambao hawawezi kumtupa leo wala kesho nawe wanakusupport kwa heshima yake.

3. Tambueni muziki wenu mnaoufanya ni bubblegum na Mnahit kwa Huruma ya Mashabiki... Lakini wapo ambao Wafanya vizuri kwa Muziki wao mzuri...Na mfahamu fika hawa ndio wanaowanyosha Mitaani ASLAY, ALIKIBA, WCB, CHEGE, BEN POL, BEKA FLAVOUR, BARNABA, MADEE, WEUSI, ROSTAM nk wanawanyoosha haswa kwenye Bodaboda, Vijiwe na kwenye Media watu wanarequest sana ngoma zao.

4. Tambueni kufanya Interview sio mpaka muwe na Ngoma mpya... Wakati mwingine mnaweza kuzungumzia hata mwenendo wa gemu, tathmini ya ngoma zenu kimapokezi na mnawezaje kuvunja tabaka la wasanii niliowataja hapo kwanini wao tu wanapenya.

5. Kuna siku nilitumiwa SMS na Mtangazaji kutoka Mkoa Fulani.. Akaniuliza Swali kaka wapi unapata kirahisi Sauti za Wasanii na zipo Clear... Nikamweleza namna navyopambana nao akaniambia naomba ukiwa unawatumia maswali unanishtua wajibu na yake coz wanadharaulika.

NB:- MFAHAMU kuwa Mashabiki wa Mikoani sio Washamba kiasi hicho... Naomba Msiwe mnasumbua sasa.. Ikifika msimu wa Matamasha mnataka kuwepo kwenye List au tuwaandalie Show.. Mnapiga sana simu mpaka tunashindwa kuongea na watu wa madili na wapenzi wetu.. Fanyeni muziki Dar Es Salaam na show fanyeni huko huko.. Endeleeni tu!

Imeandikwa na Chris Bee.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: