Mbunge wa Jimbo la Nkenge leo amekabidhi vifaa vya michozo vyenye thamani ya shilingi milioni 36,080,000 za kitanzania kwa shule zote za sekondari zilizo ndani ya Wilaya ya Missenyi na timu za mpira za kata 13 zilizomo jimboni Nkenge
Vifaa hivyo vimekabidhiwa katika mkutano mkubwa wa kila mwaka wa Wadau wa maendeleo wa Jimbo la Nkenge uliofanyika jana Alhamisi Dec 14, 2017 katika ukumbi wa Halmashauri ya Missenyi-Bunazi.
Akiongea na wadau Balozi Dk. Kamala amesema; 'anaomba vifaa hivyo vitunzwe kama ilivyokusudiwa pia ametumia fursa hiyo kutoa shukrani kwa Ubalozi wa Ubeligiji Tanzania, Chama cha Mpira cha Ubeligiji kwa kusaidia kupata Vifaa hivyo pia amekishukuru kiwanda cha Kagera Sugar kwa kusaidia kusafirisha vifaa hivi kutoka Dar es Salaam mpaka Missenyi jimboni mwake.
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: