Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya Chadema, Mch. Peter Msigwa amewataka wananchi wa Iringa Mjini kumchomea nyumba anayoishi pamoja na magari yake endapo atahama Chama cha Demokrasia na Maendeleo na kuhamia CCM.

Msigwa amefunguka hayo wakati akituma salamu kwa wale ambao wamekuwa wakimrubuni kuhamia CCM na kusema kwamba heshima na dhamana aliyopatiwa na wananchi wa Manispaa ya Iringa ni kubwa mno hivyo kufanya hivyo ni kuuza hadi utu wa wapiga kura.

Akizungumzia kuhusu alivyokuwa akirubuniwa, Msigwa amesema "Walianza kunipigia kwa kujifanya marafiki zangu na baadae wakaanza kunipanga na kunirubuni kwamba Mzee ananikubali na wala hana shida na mimi hivyo nikiingia CCM nitapata nafasi, nimewakemea na nimeonya wasinipie simu na sasa hivi wameacha ila naahidi wakinipia tena nitawarekodi niwaanike hadharani" I am not that 'cheap' wakatafute wengine," Msigwa ameweka wazi.

Aidha Msigwa amefafanua kwamba hakuuingia bungeni kwasababu anahitaji pesa kwani hata kama asingekuwa Mbunge angeweza kuwa Mkurugenzi wa makampuni na kuongeza kwamba alikuwa na maisha hata kabla ya kuwa mwanasiasa na mbunge.

"Sikuingia Bungeni kwa ajili ya pesa, sipo tayari kurubuniwa kwa maneno matamu wala fedha au ushawishi kuuza utu ambao wananchi wa manispaa ya Iringa wamenipa. Ukiniangalia kwani nashindwa kuwa CEO, naweza kuwa Mkurugenzi wa kampuni yoyote. Mimi nilikuwa na maisha kabla ya kuingia hta bungeni. Sisi bado tupo imara....wacha hivi vivulana viondoke sisi ambao tunajua nini tunakutaka bado tupo imara ndani ya chama" Msigwa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: