Na Kajunason/MMG.

Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania, Mhe. John Shibuda ametema cheche baada ya kupewa kutoa salamu zake wakati wa Mkutano wa Mkuu wa Tisa wa Chama cha Mapinduzi mjini Dodoma.

Salamu zake zilikuwa na ujumbe usemao;

1. Watanzania Tuamke na Tuzinduke tuende na mwanga wa mawazo ya fikra za ukombozi za maono aminifu ya uzalendo na ya kauli na vitendo vya maslahi ya Utaifa kwa nchi yetu za Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

2. Uhuru na Haki za kila mwananchama wa Chama Chochote wa kuhamia mahali popote kama ilivyo ruksa kwa raia yeyote kwenda kuishi mahali popote.

Naomba kusema ya kwamba, hakuna mwanachama yeyote amebinafsishwa na kuwa mtwana wa kulazimishwa kuishi eneo ambalo anaona hapati msako wa kumlishia na kupata furaha yake... wale wote ambao wanahama kutoka chama kimoja kwenda kingine, wanatimiza haki zao, uhuru wao na wala wasiitwe wasaliti maana 'Taa ya Koroboi haiwezi kumulikia taa ya Umeme,'.

Nasaha zake pia alizitoa kwa kusema kuwa "Ukiwa ndani ya Nyumba unajua uchafu uliopo na ukiwa na nyumba ambayo paa lake limetoboka dawa yake ni kung'oa mabati ambayo yanasababisha kuvuja, kwa hiyo Mhe. Rais Dkt. Magufuli nakupongeza kwa kazi unayoifanya ya kubandua mabati yenye uchovu na yenye vitobo ili nyumba yetu iwe salama... Hongeza sana kwa juhudi zako zote kwa niaba ya vya vyote vilivyoshiriki.

Ujumbe wa Mwisho aliutoa, "Duniani kote wasema ukweli huchukiwa sana na wapenda uongo ambao husadifu ukweli mbandia wa kupotosha maslahi ya jamii, maslahi ya Uchumi na Taifa... Nawasifu CCM kwa kutuletea Mhe. Dkt. Magufuli kuwa mwenyekiti na kugombea na sasa ni rais wetu anayetetea maslahi ya nchi.

Nasaha zake kwa wanasisia, "Nawaomba wanasiasa kuwa Wazalendo wanashiriki katika sherehe za kumbukumbu zote...ikiwa mkristo unashiriki sherehe za kuzaliwa Bwana Yesu Kristo, ukiwa muislamu unashiriki sherehe za kuzaliwa mtume Mohammed kwanini ususie kushiriki sherehe za mapinduzi ya Zanzibar???, Kwa nini ususie sherehe za uhuru wa Tanzania???, nimelisema hili ili kuwakumbusha maana ya Uzalendo Wetu.

Vile vile alitoa wito kwa vyama vya siasa kuwa vinashiriki katika chaguzi mbali mbali ambazo zimekuwa zikifanyika za marudio... Aliomba vyama vya siasa visivyopewa ruzuku zipewe ruzuku ili viweze kujiendesha, "Mhe. Rais Dkt. Magufuli Jeshi la Simba aliwezi endeshwa na Kondoo,"
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: