Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli akifungua Mkutano Mkuu wa tisa wa CCM, katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete, Dodoma, leo. Pamoja na mambo mengine kuhusu mageuzi ndani ya Chama, uadilifu na usimamizi wa mali za Chama ili Chama kisitegemee wafadhili wakiwemo matajiri wachache, amemtaka Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana kuendelea kumsaidia katika nafasi hiyo ya Katibu Mkuu katika kipindi kingine cha miaka mitano
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimsalimia Balozi wa China hapa nchini Wang Ke, alipokuwa akisalimia mabalozi kutoka nchi mbalimbali ambao wamehudhuria Mkutano huo.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akiandaa mazingira ya kuchangamsha ukumbi kabla ya mkutano huo kuanza. Kushoto ni katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga
Wanakwaya wa TOT wakiimba wimbo maalum wa kumkaribisha ukumbini Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk John Magufuli
Wajumbe wakijimwayamwaya ukumbini kushangilia wakati Mwenyekiti wa CCM Taifa, akiingia ukumbini
Mwimbaji wa TOT akiimba wimbo wa kuhamasisha mapokezi ya Mwenyekiti ukumbini.
Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Jakaya Kikwete na Mwenyekiti mstaafu wa CCM Ali Hassan Mwinyi wakimsubiri Mwenyekiti Kuingia Ukumbini. Mzee Mwinyi akisoma toleo maalum la gazeti la Uhuru wakati akisubiri.
Mwenyekiti wa CCM Rais Dk John Magufuli akisalimia viongozi mbalimbali baada ya kuingia ukumbini. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein na kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana
Mwenyekiti wa CCM Rais Dk John Magufuli akiwa tayari ukumbini. Wengine kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mstaafu Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Makamu Mwenyekiti wa CCM Rais wa Zanzibar Dk. Shein, Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti wa CCM-bara Philip Mangula na Mwenyekiti Mstaaafu wa CCM Benjamin Mkapa.a
Mwenyekiti wa CCM Rais Dk John Maguduli akijadili jambo na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana baada ya kuketi ukumbini.
Waimbaji wa TOT wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya Mkutano kuanza.
Wajumbe wakiwa wamesimama kuimba wimo wa Taifa.
Mwenyekiti wa CCM Rais Dk John Magufuli na viongozi wengine meza kuu wakiimba wimbo wa Taifa huku wamesimama kwa ukakamavu.
Viongozi wakiw wameketi baada ya kuimba wimbo wa taifa.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimkaribisha Mwenyekiti kufungua Mkutano huo.
Wapicha picha wakifuatilia matukio.
Mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere Mama Maria Nyerere akiwa na Mama Salma Kikwete kwenye mkutano huo
Baadhi ya wageni waalikwa na wajumbe wakiwa kwenye mkutano huo
Mwenyekiti wa CCM Rais Dk Magufuli (kulia)akifungua mkutano huo mkuu
Wajumbe wakishangilia baada ya Mwenyekiti wa CCM Rais Dk Magufuli kumtaka Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kuendelea kumsaidia katika nafasi hiyo ya Ukatibu Mkuu kwa miaka mingine mitano.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiinuka kuonyesha ishara ya kukubali makakwa ya Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. Magufuli. Kulia ni Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Zanzibar Dk Amani Abeid Karume na Mzee Mkapa ambaye anacheka kuonyesha kuunga mkono.
Baadhi ya waliohamia CCM kutoka vyama vya upinzani wakisimama baada ya kutmbulishwa na Mwenyekiti wa CCM Rais Dk Magufuli kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM Rais Dk Magufuli akipongezwa na Mwenyekiti mstaafu wa CCM Jakaya Kikwete baada ya hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Bara Pius Msekwa
"Hotuba imeshiba" inaelekea ndivyo Kikwete alivyomwambia Dk Magufuli baada ya kumpongeza.
Mwenyekiti wa CCM Dk Magufuli akirudi katika nafasi yake baada ya kutoa hotuba na kufungua mkutano huo
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akitoa maelezo kuhusu CCM ilivyotekeleza kazi zake katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. kabla ya hapo alitumia fursa hiyo kumshukuru Mwenyekiti wa CCM Dk Magufuli kwa kumwamini tena ili aendelee kumsaidia. Kinana amemwahidi kumsaidia kwa weledi na uaminifu mkubwa.
TOT wakimshangilia Mwenyekiti Dk. Magufuli baada ya hotuba yake. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: