Tuesday, December 19, 2017

MZEE CHEYO AWATOLEA UVIVU WANASIASA WANAOENEZA SIASA ZA CHUKI

Na Kajunason/MMG.

Mzee John Cheyo mapema Disemba 18, 2017 mjini Dodoma katika mkutano wa Tisa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) amewatolea uvivu wanasiasa wanaoeneza siasa za chuki kwa kutoa matusi dhidi ya vyama vingine.

Alianza kwa kusema haya;

Ndugu zangu wanaCCM, Najua kesho nitashambuliwa magazetini kwa kusema mimi ni ndugu yenu, nimezungumza hivi makusudi kabisa mimi ni muumini kabisa wa msimamo wa siasa si uadui' na mara nyingi nakufatilia katika hotuba zako kuwa "Wewe ni rais wa wote, maendeleo hayana Chama. Ninawasihi wenzangu wanaoshindana na CCM, wajue kwamba...LiCCM linatisha. Tusitumie muda mwingi kuliangusha, na ukitaka kuliangusha na wewe ujue umekaa wapi?? Lisije kukuangukia usije ukapotea kabisa...

Lazima tukubali sisi wote ni Watanzania na mama yetu ni Tanzania na Mwanasiasa yeyote anayeishambulia Tanzania huyo ndiye adui wa Tanzania.

Mhe. Mwenyekiti naomba CCM utuongoze kufanya vyama vya siasa visiwe viwanda vya matusi, umehimiza viwanda vya watu wafanye kazi... haujahimiza ushindani wa siasa za matusi. Na nyinyi CCM mnaweza kutupa mfano na mkatisha kabisa.

CCM muendelee kutupa mfano, Tuache kususa susa kwenye chaguzi mbali mbali... Nikupongeze kwa yote ambayo umeyafanya kwa kipindi cha miaka miwili.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu